| Swahili
MICHEZO
2 dk kusoma
Rais wa FIFA asema 'hakuna shaka' Iran itashiriki Kombe la Dunia
Matamshi haya yanakuja baada ya Mexico kuthibitisha kuwa shirikisho la soka duniani, FIFA limekataa ombi la Iran kuhamisha mechi zao zote nchini Mexico.
Rais wa FIFA asema 'hakuna shaka' Iran itashiriki Kombe la Dunia
Marekani itakuwa mwenyeji wa mashabiki wa kimataifa wa Kombe la Dunia, anasema rais wa FIFA / Reuters
tokea masaa 5

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani, FIFA Gianni Infantino anasema "hakuna shaka" Iran itashiriki Kombe la Dunia 2026 licha ya vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.

"Iran itakuwepo bila shaka. Tunatarajia kufikia wakati huo hali itakuwa ya usalama, hilo litasaidia sana," Infantino alisema katika kituoc cha CNBC.

"Lakini Iran muhimu iwepo, wanawakilisha watu wao, wamefuzu, wachezaji wanataka kucheza," alisema kuhusu mechi zao zilizoratibiwa kuchezwa Marekani mwezi Juni.

Alisema kuwa "michezo haitakiwa kufungamanishwa na siasa."

"Kama hakuna mtu mwingine anayeamini katika kuunganisha watu, sisi tunalifanya hilo," aliendelea.

Matamshi yake yanakuja baada ya Mexico kuthibitisha kuwa FIFA imekataa ombi la Iran kuhamisha mechi zake zote kwa majirani wa Marekani wa kusini.

Wasiwasi wa kutoshiriki

Kumekuwa na wasiwasi wa Iran kushiriki kwenye mashindano hayo ya dunia kutokana na vita na Marekani na Israel vilivyoanza Februari 28.

Iran ilifuzu kwa Kombe la Dunia 2026 mwezi Machi 2025 baada ya sare ya 2-2 dhidi ya Uzbekistan.

Kombe la Dunia, lina wenyeji wenza Marekani, Mexico na Canada, na linaanza Juni 11.

Hata hivyo, Iran imeratibiwa kucheza mechi zake zote za kundi G — dhidi ya Ubelgiji, Misri na New Zealand — nchini Marekani.

Kulingana na ratiba za mechi kwenye mtandao wa FIFA, Iran inatarajiwa kucheza dhidi ya New Zealand Juni 15 katika uwanja wa Los Angeles, Ubelgiji Juni 21 katika uwanja huohuo, na dhidi ya Misri Juni 26 katika uwanja wa Seattle.

CHANZO:TRT World and Agencies