| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Idadi ya vifo vya Ebola nchini DRC vyavuka 500
Idadi ya vifo vilivyotokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini DRC, sasa vimefikia zaidi ya 500.
Idadi ya vifo vya Ebola nchini DRC vyavuka 500
Wiki iliyopita, Shirika la Afya Duniani (WHO) likisema kuwa virusi adimu vya Bundibugyo vinaendelea kusambaa nchini humo./Picha:Reuters / Reuters

Idadi ya vifo vilivyotokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini DRC, sasa vimefikia zaidi ya 500.

Kulingana na takwimu iliyotolewa na Wizara ya Afya ya nchini humo, maambukizi yaliyothibitishwa hadi sasa yamefikia 1,561, ikiwemo vifo 506.

Wizara hiyo, imeongeza kuwa watu wagonjwa wapatao 253 wamepona ugonjwa huo huku wengine 628 wakiendelea kuwa chini ya uangalizi maalumu mahospitalini.

Kulingana na Wizara ya Afya ya DRC, mlipuko wa Ebola umeathiri vituo 36 vya afya katika maeneo ya Ituri na Kivu Kaskazini.

Wiki iliyopita, Shirika la Afya Duniani (WHO) likisema kuwa virusi adimu vya Bundibugyo vinaendelea kusambaa nchini humo.

Takwimu zinaonesha kuwa, jimbo la Ituri limeathirika zaidi likiwa na asilimia 91 ya maambukizi yote, na vifo vinavyofikia asilimia 84.

 

CHANZO:AFP