Siziba: Vazi la Zambia lililopata umaarufu pamoja na lile la Ghana la Fugu

Vazi la Siziba limepata umaarufu katika mitandao ya kijamii huku kukiwa na mapishano kati ya raia wa Ghana na Zambia kuhusu mavazi yao.

By
Siziba hutengenezwa kutumia vitenge, ambavyo ni vitambaa imara, vinavyotengezwa kuwa kutumia pamba./ Wengine / Others

Nchini Zambia, mavazi ya Siziba na Musisi ni ishara ya ukubwa.

Wanaume wao huvaa Siziba, huku wanawake hupendeza kwa kuvaa Musisi, pamoja na vilemba kichwani.

Mavazi haya ya asili, kwa wanaume na wanawake, yanatengezwa kwa kutumia vitenge, ambavyo ni vitambaa imara, vinavyotengezwa kuwa kutumia pamba.

Rangi zake zinazopendeza, na urembo wake unatoa simulizi ya nguvu, amani, na hadhi katika jamii, ikiashiria nguvu, huku rangi ya buluu ikiashiria utulivu, na nyeupe amani.

Siziba na Musisi ni zaidi ya mavazi; ni ushuhuda wa utajiri wa tamaduni na historia kwa Zambia.

Siziba asili yake ni Ufalme wa Lozi Magharibi mwa Zambia na kutokana na utamaduni wao, huvaliwa na watu wenye nafasi katika jamii hasa wakati wa shughuli muhimu kama vile sherehe ya kila mwaka ya Kuomboka, ambayo inaashirika mwisho wa msimu wa mvua.

Hata hivyo, vazi hilo hivi sasa linavaliwa na raia wote wa Zambia kutoka jamii na maeneo tofauti, na kuwa utambulisho wa taifa ambao umeingizwa katika fasheni ya kisasa.

Umuhimu wa Utamaduni

Katika siku za hivi karibuni, Siziba imepata umaarufu zaidi katika mitandao ya kijamii kufuatia mzaha unaoendelea kati ya Waghana na Wazambia.

Mjadala ulitiibuliwa na muonekano wa Rais wa Ghana John Mahama akiwa katika vazi la kitamaduni maafuru Fugu, ilikuwa ni katika moja ya ziara zake nchini Zambia kati ya Februari 4 hadi 6.

Baadhi ya raia wa Zambia, walifanya mzaha na kuliita vazi hilo "blauzi."

Hali hiyo iliwafanya raia wa Ghana, ikiwemo wabunge wa nchi hiyo, kuonesha vazi hilo la Fugu kupitia mitandao ya kijamii, huku Wazambia nao wakionesha Siziba.

Majibizano hayo yalibadilisha mwelekeo na kuchukua ule wa kisiasa pale Rais wa Zambia Hakainde Hichiliema alipotangaza kuwa nchi yake itaagiza Fugu kutoka Gaza.

Nae Rais wa Ghana Mahama akiashirika kupeleka nguo hizo kwa wingi nchini Zambia.

Akielezea umuhimu wa vazi hilo la Fugu katika siasa na tamaduni za Ghana, Mahama alisema vazi hilo lilivaliwa na baba wa taifa wa Kwame Nkrumah katika siku ya uhuru wa nchi mwaka 1957, na kwamba na yeye kwa fahari kubwa alilivaa vazi hilo akiwa Umoja wa Mataifa hivi karibuni.

Huku mjadala ukiendelea, kitu kimoja kiko wazi. Majibizano kupitia mitandao ya kijamii yamefanya mavazi hayo ya Fugu na Siziba kuwa maarufu na kuonesha hamu kubwa ya utamaduni na urithi wa Afrika.