Jeshi la Polisi la Brazil, siku ya Jumatano limefanya upekuzi kwenye nyumba ya kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Jair Bolsonaro, ambaye yupo kwenye kizuizi cha nyumbani kwa sasa.
Kiongozi huyo, mwenye umri wa miaka 71, anatumikia kifungo cha miaka 27 jela kufuatia jaribio lake la kufanya mapinduzi ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Rais Luiz Inacio Lula da Silva, mwaka 2022.
Wiki iliyopita, Mahakama Kuu ya Brazil, iliongeza muda wa kifungo cha nyumbani kwa Bolsonaro, kutokana na sababu za kiafya.
Hata hivyo, polisi hawakukuta silaha yoyote baada ya upekuzi huo, kulingana na mwanasheria wa kiongozi huyo wa zamani, Joao Henrique Nascimento de Freitas.
Upekuzi huo, uliodumu kwa takribani saa moja, ulihusisha chumba cha binti wa kiongozi huyo, ambaye alikuwa amelala kwa wakati huo.
















