| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan aadhimisha Siku ya Maji Duniani, atahadharisha uhaba wa maji
Mke wa Rais ametaka kuwepo kwa uelewa zaidi na ufanisi huku hatari ya uhaba wa maji ikiongezeka duniani.
Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan aadhimisha Siku ya Maji Duniani, atahadharisha uhaba wa maji
Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan akihutubia wakati wa iftar katika makao makuu ya AK Party jijini Istanbul, Uturuki, Machi 22, 2026. / AA Maktaba / TRT Afrika Swahili
tokea masaa 16

Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan ameadhimisha Siku ya Maji Duniani kwa kutaka jitihada zaidi kuhakikisha upatikanaji wa maji na kutadharisha kwamba maji yamekuwa ni uhai wa kitaifa, ulinzi na upatikanaji wa chakula kwa nchi duniani.

Katika ujumbe uliotolewa Jumapili kupitia mtandao wa kijamii wa Uturuki NSosyal, Emine Erdogan amesema nchi zote hivi sasa zinakabiliwa na changamoto inayohusiana na uhaba wa maji.

“Kwa kukusanya mawazo yetu, jitihada na malengo mema, tunaweza kuzuia nchi yetu kuwa miongoni mwa zile zinazokabiliwa na uhaba wa maji," amesema.

Mke wa Rais pia ametaka kuwepo kwa uelewa ya maji na kuwataka watu wote kuchukua hatua ya "uaminifu kwa maji, heshima ya baraka na maisha," na kutoa hamasa ya kitaifa kuhusu matumizi ya maji.

Siku ya Maji Duniani, inaadhimishwa kila mwaka Machi 22, inataratibiwa na Umoja wa Mataifa kujenga uelewa kuhusu matumizi ya maji endelevu.