| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Uturuki na mataifa mengine yalaani shambulizi la Houthi dhidi ya Mecca
Mataifa kadhaa yametaka kusitishwa kwa mashambulizi ya aina hiyo.
Uturuki na mataifa mengine yalaani shambulizi la Houthi dhidi ya Mecca
Mataifa kadhaa yametaka kusitishwa kwa mashambulizi ya aina hiyo.

Uturuki imelaani vikali shambulizi lililofanywa na Houthi, likilenga mji mtakatifu wa Mecca uliopo Saudi Arabia.

“Tunalaani vikali shambulizi hilo,” ilisema Uturuki kupitia taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo siku ya Jumatano.

Wakati huo huo, Uturuki imetaka kusitishwa kwa mashambulizi kama hayo, ikitadhaharisha kuwa yanafifisha usalama wa kanda.

Hali kadhalika, Uturuki imezitaka pande zinazohasimiana, kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa kanda.

“Ni vyema kulinda usalama wa Mecca kwa umuhimu wa jumuiya ya Kiislamu ulimwenguni,” alisema Mkuu wa Mawasiliano wa Uturuki, Burhanettin Duran kupitia taarifa hiyo.

Mapema, jeshi la anga la Saudi Arabia, lilifanikiwa kutungua na kuharibu droni hizo, kabla hazijaingia anga la Mecca.

Kwa upande wake, kikundi cha Houthi cha Yemen, kilikana kuhusika na jaribio la shambulizi hilo.

Saudi Arabia

Saudi Arabia imekielezea kitendo hicho kuwa ni cha kioga, likiapa kuchukua hatua stahiki za kulinda mji huo mtakatifu.

Qatar

Kwa upande wake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, imeliita jairbio hilo, kama kitendo cha aibu.

Palestina

Rais wa Palestina kwa upande wake, alionesha mshikamano na Saudi Arabia, dhidi ya matishio ya usalama na utulivu wake.

CHANZO:TRT World and Agencies