| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Wabunge wa Ufilipino wajiandaa kumng’oa madarakani Makamu wa Rais Sara Duterte
Sara, ambaye ni binti wa rais wa zamani wa nchi hiyo Rodrigo Duterte, anakabiliwa na tuhuma za ufisadi na jaribio la kutaka kumuua mshirika wake wa zamani na kiongozi wa zamani wa taifa hilo, Ferdinand Marcos.
Wabunge wa Ufilipino wajiandaa kumng’oa madarakani Makamu wa Rais Sara Duterte
Makamu Rais wa Ufilipino, Sara Duterte./Picha:Reuters

Wabunge wa Ufilipino, siku ya Jumatatu walipiga kura ya kumwondoa madarakani Makamu Rais wa nchi hiyo Sara Duterte, mchakato ambao utatia dosari lengo lake la kugombea urais mwaka 2028.

Sara, ambaye ni binti wa rais wa zamani wa nchi hiyo Rodrigo Duterte, anakabiliwa na tuhuma za ufisadi na jaribio la kutaka kumuua mshirika wake wa zamani na kiongozi wa zamani wa taifa hilo, Ferdinand Marcos.

"Hili sio suala la kisiasa bali ni suala la dhamiri na mustakabali wa taifa letu,” alisema Bienvenido Abante mmoja ya wabunge hao.

Jumla ya kura 255 zilipigwa siku ya jumatatu kwa lengo la kumuondoa madarakani mwanasiasa huyo.

Sara Duterte anatuhumiwa kuwahonga baadhi yta maafisa wa serikali nchini humo na jaribio la kumuua Marcos, ambapo anadaiwa kumkodi mtu wa kutekeleza mauaji hayo.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu, upande wa utetezi wa Duterte ulidai kuwa ushahidi wote unabakia kwa wanaomtuhumu mwanasiasa huyo.

"Tuko tayari kumtetea Makamu wa Rais kabla ya bunge le seneti kukaa na kujiandaa kumng’oa madarakani," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

CHANZO:AFP