| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Mchango wa sekta ya madini Tanzania wapongezwa kimataifa
Kwa mujibu wa Ripoti ya Uwekezaji Tanzania ya Mwaka 2025, thamani ya mtaji wa uwekezaji katika Sekta ya Madini imeongezeka hadi kufikia dola za Marekani bilioni 9.79 kwa mwaka 2024, kutoka dola bilioni 9.15 za mwaka 2023
Mchango wa sekta ya madini Tanzania wapongezwa kimataifa
Waziri wa Madini wa Tanzania, Anthony Mavunde./Picha:@MadiniTanzania / Others

Nchi jirani zimeimwagia sifa Tanzania kufuatia mchango wa sekta madini wa nchi hiyo katika kukuza pato la taifa (GDP), huku nchi jirani hizo, zikielezea nia ya kujifunza mafanikio ya usimamizi wa sekta hiyo.

Wakizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji wa Madini unaofanyika jijini Nairobi, mawaziri mbalimbali wa madini wa Afrika walitambua hatua kubwa zilizopigwa na Tanzania katika kuifanya sekta ya madini kuwa mhimili wa uchumi.

Waziri wa Madini wa Kenya Hassan Ali Joho,  ameitaja Tanzania kama mfano bora wa kuigwa kikanda, akisisitiza umuhimu wa kukuza na kuimarisha sekta ya madini barani Afrika.

Kwa upande wake, Waziri Waziri wa Petroli na Rasilimali Madini wa Somalia Dahir Shire Mohamed, amesema kuwa serikali yake inaichukulia Tanzania kama mfano halisi katika kujenga mifumo imara ya usimamizi wa rasilimali madini.

 Akizungumza katika mdahalo maalum wa mawaziri hao, Waziri wa Madini wa Tanzania, Anthony Mavunde, amesema mafanikio hayo yametokana na uongozi thabiti wa kiongozi wa nchi hiyo, Samia Suluhu Hassan, ambaye  kwa mujibu wa waziri huyo, ameweka mazingira wezeshi ya  uwekezaji, kuimarisha usimamizi wa rasilimali, na kusukuma mbele ajenda ya kuongeza thamani ya madini.

Hapo awali, wakati akifungua mkutano huo, Rais William Ruto wa Kenya, amezitaka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na bara zima la Afrika, kuunganisha nguvu katika kuongeza thamani ya rasilimali madini ili kuongeza tija na ushindani wa ukanda huo katika soko la dunia.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Uwekezaji Tanzania ya Mwaka 2025, thamani ya mtaji wa uwekezaji katika Sekta ya Madini imeongezeka hadi kufikia dola za Marekani bilioni 9.79 kwa mwaka 2024, kutoka dola bilioni 9.15 za mwaka 2023 na dola bilioni 8.64 za mwaka 2022.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Soma zaidi
Rais wa Afrika Kusini aagiza hatua za kuwalinda wanawake kufuatia mfululizo wa mauaji
Misri yakana kuingilia mambo ya ndani ya Ethiopia na kuunga mkono makundi yenye silaha
Edward Kijanangoma atawazwa mfalme mpya wa Tooro
Je, Afrika itapata viti vya kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa?
Jeshi la Polisi Tanzania laonya wanaochochea mgomo wa madereva wa mabasi
Madaktari bingwa wa Tanzania waweka kambi ya matibabu Malawi
Makamu wa Rais Tanzania ataka vijana kupewa fursa za mafunzo ya ajira
Jeshi la Sudan lapinga madai ya kuunga mkono makundi ya upinzani Ethiopia
Uchaguzi Mkuu kurejesha utulivu Sudan Kusini?
Marekani italazimika kuondoka Mashariki ya Kati: Iran
Mashambulizi ya kigaidi mjini Mogadishu yapungua kwa karibu asilimia 90: Serikali ya Somalia
Maambukizi ya Ebola nchini DRC ni zaidi ya 8,000 tangu kuanza kwa mlipuko huo
Watoto 17 miongoni mwa wahamiaji 250 waliookolewa katika pwani ya Mauritania
Marekani kusitisha ufadhili wa sekta ya afya nchini Zimbabwe kufikia mwishoni mwa mwezi wa Septemba
Mwanamke wa kumi apatikana amefariki katika msururu  wa mauaji nchini Afrika Kusini
Qatar Airways yakopesha marubani kwa shirika la ndege la taifa la Rwanda
Wapiganaji wa RSF wahamia upande wa jeshi la Sudan baada ya kushuhudia 'maafa'
Mkuu wa Umoja wa Mataifa asikitishwa kwa kunyimwa viza  kiongozi wa Sudan, Burhan kuhudhuria UNGA
Jenerali wa DR Congo miongoni mwa watu 13 waliofariki katika ajali ya ndege
Afrika itapata hadhi ya uwanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa?