Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan, siku ya Ijumaa amehudhuria ufunguzi wa mkutano wa mawaziri wa G20, uliofanyika nchini Marekani.
Wakati wa mkutano huo, Fidan alikutana na waziri mwenzake kutoka Indonesia, Arrmanatha Nasir na Toshimitsu Motegi wa Japan.
Mkutano huo, ambao uliandaliwa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Marco Rubio, umewaleta pamoja wanadiplomasia kujadili changamoto za kiulimwengu, nishati, usalama wa chakula na mambo mengine.
Pia, mkutano huo ni maandalizi ya mkutano wa wakuu wa G20, utakaofanyika Disemba 14 hadi 15, jijini Miami nchini Marekani.
CHANZO:Anadolu Agency




























