Rais wa Somalia awasili Uturuki kwa mazungumzo na Rais Erdogan

Majadiliano hayo yanatarajiwa kuangazia uhusiano baina ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali na mivutano ya hivi punde iliyosababishwa na Israel kulitambua kwa upande mmoja eneo lililojitenga la Somalia la Somaliland.

By
Rais Hassan Sheikh Mohamud akiwasili Istanbul. / AA / AA

Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, amewasili nchini Uturuki kwa mazungumzo na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan, jijini Istanbul.

Mazungumzo yanatarajiwa kuzingatia uhusiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali pamoja na mvutano wa hivi karibuni ulioibuliwa na utambuzi wa upande mmoja wa Israel wa eneo la Somalia linalotaka kujitenga, Somaliland, kama taifa huru, jambo ambalo limevakwa na hasira na malalamiko makubwa kimataifa.