| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Jeshi la Sudan lakomboa vijiji vitatu karibu na Kordofan Magharibi kutoka kwa RSF
Jeshi la Sudan na vikosi washirika vilidhibiti maeneo matatu na vijiji kadhaa mashariki mwa Al Nuhud katika jimbo la Kordofan Magharibi siku ya Jumamosi, vyanzo vya kijeshi vililiambia shirika la Anadolu.
Jeshi la Sudan lakomboa vijiji vitatu karibu na Kordofan Magharibi kutoka kwa RSF
Mapigano kati ya jeshi la Sudan na RSF yameongezeka makali katika majimbo ya Kordofan Kaskazini, Magharibi na Kusini tangu 25 Oktoba 2025. / AFP / AFP

Jeshi la Sudan na vikosi washirika vilidhibiti maeneo matatu na vijiji kadhaa mashariki mwa Al Nuhud katika jimbo la Kordofan Magharibi siku ya Jumamosi, vyanzo vya kijeshi viliambia shirika la Anadolu.

Vyanzo hivyo vilisema jeshi liliteka maeneo ya Khamasat, Markab na Umm Oweisha na kuendelea kusonga mbele kuelekea Al Nuhud, mji wa pili kwa ukubwa katika jimbo hilo, ambao bado unadhibitiwa na kundi la wanamgambo la Rapid Support Forces (RSF).

Askari wa jeshi na wapiganaji washirika walisambaza video kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha wanajeshi wakiingia katika maeneo ya Khamasat na Umm Oweisha.

Maafisa wa Sudan walisema jeshi na vikosi washirika viliteka Al Khuway, eneo lililo umbali wa takriban kilomita 100 kutoka Al Nuhud, siku ya Ijumaa kufuatia mapigano na kundi la RSF.

Vita vya uharibifu mkubwa

Mnamo Novemba 7, jeshi pia liliteka Ayal Bakhit, kaskazini-magharibi mwa Al Khuway, baada ya mapigano na kundi la wanamgambo la RSF, vyanzo vilivyo na ufahamu kuhusu mapigano hayo viliambia Anadolu.

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na kundi la RSF yameongezeka makali katika majimbo ya Kordofan Kaskazini, Magharibi na Kusini tangu Oktoba 25 mwaka jana.

Mgogoro huo, ambao ulizuka mwezi Aprili 2023, umesababisha vifo vya makumi ya maelfu ya watu na kuwafanya karibu watu milioni 13 kuyahama makazi yao, kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa.


CHANZO:َAA