| Swahili
MICHEZO
2 dk kusoma
Timu ya wasichana ya Tanzania ya chini ya umri wa miaka 15 imetwaa ubingwa wa CECAFA
Mashindano hayo ya kanda ya CECAFA huwakutanisha timu za wasichana U-15 kutoka kote kanda hiyo, huku washindi wakipata haki ya kuiwakilisha CECAFA katika michuano ya ngazi ya bara ya CAF African Schools Football Championship.
Timu ya wasichana ya Tanzania ya chini ya umri wa miaka 15 imetwaa ubingwa wa CECAFA
Tanzania imeshiriki fainali za CAF African Schools Championship mara mbili; / TRT Afrika

Timu ya wasichana ya Tanzania U-15 imeifunga Kenya na kutwaa taji la CECAFA, huku ikijihakikishia nafasi katika michuano ya CAF African Schools Football Championship ya msimu wa 2026-27.

Tanzania iliifunga Kenya, iliyoshika nafasi ya pili, kwa mabao 3-0 katika mechi kali iliofanyika Kigali, Rwanda, kupitia kwa washambuliaji Salah Msagala, Anna Pascal na Eva Maiope.

Ushindi huo unaipatia Tanzania zawadi ya dola 100,000.

Kwa upande mwingine, Kenya imepata zawadi ya kujifariji ya dola 75,000, ikifuatiwa na Uganda iliyoshika nafasi ya tatu na kupata dola 50,000.

Ushindi uliotangulia

Timu ya Tanzania iliingia fainali baada ya kuifunga Uganda mabao 2-0 katika nusu fainali, ambapo Debora Salala na Salah Msagala walifunga mabao hayo kwa ajili ya mabingwa hao watetezi.

Kenya ilifika fainali baada ya kuwaondoa wenyeji Rwanda kwa mikwaju ya penalti kufuatia sare katika muda wa kawaida wa mchezo.

Mashindano hayo ya kanda ya CECAFA huwakutanisha timu za wasichana U-15 kutoka kote kanda hiyo, huku washindi wakipata haki ya kuiwakilisha CECAFA katika michuano ya ngazi ya bara ya CAF African Schools Football Championship.

Sasa Tanzania itaiwakilisha CECAFA katika michuano ya CAF African Schools Championship dhidi ya washindi wa kanda nyingine tano: Cosafa, WAFU A, WAFU B, UNAF, na UNIFAC.

Tanzania imeshiriki fainali za CAF African Schools Championship mara mbili; mara ya kwanza ikiwa ni msimu wa 2022-23 jijini Durban, Afrika Kusini, ambapo ilitwaa taji la kwanza kabisa la wasichana kwa kuifunga Morocco mabao 3-0 katika fainali.

Mwaka uliofuata (2023-24), ilifuzu moja kwa moja kwa kuwa mwenyeji lakini ilimaliza katika nafasi ya nne nyuma ya Uganda katika hatua ya mchujo. Afrika Kusini iliifunga Morocco na kutwaa ubingwa huo.

Ubingwa wa msimu wa 2024-25 ulienda kwa Ghana, ambayo iliifunga Morocco katika fainali, huku Afrika Kusini ikishika nafasi ya tatu. Mashindano hayo ni sehemu ya mpango wa CAF wa kukuza vipaji vya vijana, unaolenga kulea vipaji vya soka vya vijana kupitia soka la shuleni.

CHANZO:TRT Afrika