Rais Erdogan apongeza usitishaji wa mapigano nchini Syria, ahimiza suluhu ya kudumu
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameonya kuwa jaribio lolote la kuendeleza uchochezi nchini Syria kuanzia sasa “litakuwa sawa na kujitoa muhanga,” akisisitiza kuwa uthabiti lazima udumishwe.
Uturuki imepongeza usitishaji wa mapigano nchini Syria siku ya Jumanne, Rais Recep Tayyip Erdogan alisema, akieleza matumaini yake kwamba utasababisha suluhu ya kudumu bila ya umwagikaji wa damu zaidi.
Akihtubia chama chake tawala cha ‘AK Party’ bungeni siku ya Jumatano, Erdogan alisema kuwa Uturuki “tangu mwanzo kabisa imekuwa ikitetea kwa nguvu zote” kuhifadhiwa kwa Syria kama taifa moja lenye mamlaka kamili, uhuru wa mipaka yake na mshikamano wa kisiasa.
Ofisi ya Rais wa Syria ilitangaza siku ya Jumanne kwamba imefikia makubaliano na kundi la kigaidi la YPG, na kulipa kipindi cha siku nne cha kuandaa ramani ya utekelezaji wa muungano wa kiutendaji wa eneo la Hasakah, ambapo katika kipindi hicho sitisho la mapigano lingeendelea kutekelezwa. Baadaye YPG ilisema katika taarifa kwamba itatekeleza kikamilifu makubliano hayo ya usitishaji wa mapigano.
Erdogan alionya kwamba jaribio lolote la kufanya uchochezi nchini Syria kuanzia sasa “litakuwa sawa na kujtoa muhanfa,” akisisitiza kuwa uthabiti lazima ulindwe.
Alisema kuwa ujumuishaki kamili nchini Syria “utafungua ukarasa mpya,” akiongeza kuwa utulivu utanufaisha zaidi Wakurdi wa Syria.
“Hatuna nia yoyote juu ya ardhi ya nchi yoyote wala hatuingilii masuala ya ndani ya taifa lolote, lakini hatutaruhusu maslahi ya nchi yetu kudhoofishwa,” Erdogan alisema.
Rais wa Uturuki pia alisema kuwa alijadili masuala mbalimbali na Rais wa Marekani Donald Trump katika mazungumzo yao kupitia njia ya simu, yakiwemo mambo “yatakayochangia usalama wa Syria,” kama juhudi za pamoja za kupambana na Daesh.