Kwa nini mashambulizi yanaongezeka Nigeria licha ya kuwepo kwa vikosi vya Marekani?

Wachambuzi wanasema Marekani ilikurupuka na kusema ni mauaji ya halaiki dhidi ya Wakristo bila kufahamu tatizo kubwa la ugaidi nchini Nigeria.

By Charles Mgbolu
"Taarifa za Marekani zilikuwa potofu na hazikuwa na msingi wowote wa data kuhusu mzozo." / Anadolu Agency

Miezi miwili iliopita, Marekani ilifika Nigeria wakieleza kuwa ndiyo suuhu - wakitoa taarifa za kijasusi, mafunzi, na msaada wa kimkakati kusaidia katika tatizo kubwa la ugaidi. Lakini siku ya Alhamisi, kukawa na tarifa kuwa Marekani imeagiza maafisa wa ubalozi ambai kazi zao hazina umuhimu mkubwa basi waondoke nchini humo wao pamoja na familia zao, sababu ikiwa hali mbaya ya usalama.

Nchi yenye uwezo duniani ikiingia kama mkombozi alafu kuwataka maafisa wa ubalozi miezi miwili baadaye kuondoka kunazua maswali mengi ambayo baadhi ya wachambuzi wanasema yanaanza na namna suala zima la mashambulizi ya kigaidi lilivyoanzishwa.

Mchambuzi wa masuala ya usalama wa Nigeria Mubarak Aliyu anasema watu hawajui hali halisi — hasa Marekani, ambao wanadai ni ‘‘Mauaji ya halaiki dhidi ya Wakristo’’ — yametatiza zaidi mzozo huo, na sasa Marekani inakabiliwa na aibu ya kuwa vita dhidi ya ugaidi ambavyo walidhani wanadhani wanafahamu ni tofauti kabisa.

‘Simulizi potofu’

“Marekani ilishindwa kutambua na kutaja mashambulizi hayo kuwa ‘Mauaji ya halaiki dhidi ya Wakristo’ ’. Hawakufahamu namna gani tatizo la ugaidi lilivyo kubwa nchini Nigeria, na kulikuwa na tatizo la kuelewa wadau wangapi walikuwepo kwenye tatizo hilo,” Aliyu alielezea TRT Afrika.

Kulingana na mchambuzi huyo, vurugu nchini Nigeria haziwezi kutatuliwa kwa kuangalia tatizo moja, na hatari zaidi, simulizi potofu kama walivyofanya Marekani.

“Simulizi ya Marekani ilikuwa potofu na haikuwa inazingatia data zozote za mzozo,” Aliyu anasema.

Hali hiyo ya kutoelewa, anasema, huenda ikawa imefanya Marekani kufikiria kuingilia kati.

Mwishoni mwa 2025, shambulizi la Marekani ambalo walidai linalenga magaidi kaskazini magharibi mwa Nigeria, kwa mfano, bado lina utata.

“Kwa kweli hatujui ni magaidi wangapi walikatwa makali,” Aliyu anasema. “Lakini tunajuwa imeongeza hali ya taharuki. Makundi ya kigaidi yanaonekana kutumia mbinu hizi kusajili watu zaidi — yakisema, ‘hii ndiyo sababu tunapinga ushawishi wa kimagharibi.’”

Uchumi wao

Makundi yenye silaha siyo tu wahalifu wanaoendesha pikipiki lakini wamekuwa sehemu ya uchumi, mchambuzi wa masuala ya usalama, pia kutoka Nigeria, Kabiru Adamu anasema.

“Wanadhibiti migodi, wanateka watu ili walipwe kikombozi, na kukusanya kodi. Muhimu waingize mapato, inawezekana wakaendelea na mfumo huu kwa muda.”

Kulingana na uchunguzi wa Shirika la International Centre for Investigative Reporting 2025, magaidi wanadhibiti migodi haramu katika maeneo ya Majimbo ya Kaduna, Zamfara na Niger.

Kupata silaha

“Hatujajitahidi kuzuia upatikanaji wa silaha,” anasema Aliyu.

Ukuaji na ugumu wa makundi hayo uko wazi. Kando na silaha ndogo ndogo, kuna matumizi makubwa ya teknolojia. Katika miezi ya hivi karibuni, jeshi la Nigerian limetaja mashambulizi ya droni zenye silaha katika maeneo ya kaskazini mashariki.

“Makundi mengi yenye silaha yanakumbatia teknolojia, ikiwemo droni pia, kufanya mashambulizi, kufanya uchunguzi. Na serikali inaonekana kutatizika katika kukabiliana na hali hii,” Aliyu anasema.

Kuendelea kusajili watu

Huku jeshi likijivunia kupata mafanikio kuwaondoa makamanda waandamizi, Adamu anasema hili halijatoa tafsiri ya mafanikio ya muda mrefu.

“Seriklai inawaua makamanda wao, lakini haizuii usajili wa wanachama wapya. Kwa hiyo, wanaongezeka na kuunda tena mfumo mwingine.”

Hatari yake ni kuwa bila kuvunja njia yao ya kusajili watu - inayochochewa na umaskini, itikadi, na changamoto zinazowakabili — mzozo huo huenda ukawa wa kujitakiwa wenyewe.

Kutoaminiana

Mbali na mkakati na mbinu kuna suala la msingi zaidi: uaminifu.

Adamu anasisitiza kuwa usalama wa kisasa unahitaji watu zaidi — jamii ambao ziko tayari kutoa taarifa za kiintelijensia. Lakini katika sehemu nyingi za nchini Nigeria,uaminifu huo haupo.

Operesheni za kijeshi na changamoto ya kuwaua raia imefanya kuwepo kwa kutoaminiana, Adamu anaeleza.

Matokeo yake ni kukosekana kwa ‘‘taarifa za kiintelijensia kutoka kwa wananchi’’ — ambazo kwa kawaida ni muhimu sana dhidi ya ukosefu wa usalama.