Zanzibar inajiandaa kuwa na hafla ya futari kubwa zaidi duniani, ikipanga kuvunja rekodi ya sasa iliyowekwa na nchini Lebanon mwaka jana.
Rekodi ya sasa ni ya mji wa Beirut, ambapo watu karibu 5,800 walikusanyika kupata futari wakati wa Ramadhan 2025. Kisiwa hicho cha Zanzibar kinajiandaa kuwafuturisha idadi kubwa zaidi ya watu kwa wakati mmoja, kikilenga kuwa na karibu 15,000 kwa ajili ya futari.
Arif Abbas Manji, mkuu wa Tume ya Utalii Zanzibar, aliieleza hafla hiyo ya Jumamosi kama majaribiuo mazuri ya kimkakati.
"Haya ni majaribio. Tunatarajia kuwaalika maafisa wa Guinness World mwakani wakati tutakapokuwa tunafanya shughuli yenyewe halisi," alieleza.
Utalii halal
Futari hiyo itafanyika katika Uwanja wa Amaan, uliopo katika eneo maarufu la Mji Mkongwe. Uwanja huo una uwezo wa kuingia matu 15,000, ambapo waandaaji wanapanga kuujaza wote. "Tunatarajia kuwa uwanja utajaa wote," Manji amesema.
Wageni waalikwa ni ishara ya mchanganyiko wa watu kutokana matabaka mbalimbali, kutoka kwa watu wa kipato cha chini, mayatima, wanafunzi, na watalii wanaozuru kisiwa hicho.
Manji alieleza kuhusu mipango ya kuimarisha utamaduni na utalii, akieleza kuwa utalii wa halal sasa hivi unapata umaarufu duniani, hafla hiyo itakuwa fursa ya kipekee ya kula vyakula vya Kizanzibari na kufurahia utamaduni wa eneo hilo wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Zanzibar, ina wakazi takriban milioni mbili, asilimia 90 wakiwa ni Waislamu, kuufanya mwezi wa Ramadhan kuwa na umuhimu mkubwa kote visiwani humo.
















