Watu 13 wauawa katika shambulio lingine la kigaidi kaskazini mwa Nigeria

Walishambulia sehemu moja iliyokuwa na shughuli nyingi sokoni, kusababisha taharuki miongoni mwa wafanyabiashara, wakazi, anasema afisa mmoja

By
Mashambulizi nchini Nigeria. / AA

Watu wasiopungua 13 wameauawa siku ya Ijumaa katika shambulio lingine la kigaidi sokoni Jimbo la Benue kaskazini kati mwa Nigeria.

Shambulio hilo lililenga soko la Anwase huko Mbaikyor,Manispaa ya Kwande, ambapo pia waliteka nyara wanawake na kuchoma vizimba sokoni.

Ibi Andrew, msaidizi wa mwenyekiti wa Manispaa ya Kwande, anasema washambuliaji walivamia sehemu hiyo wakati wa shughuli nyingi shughuli nyingi sokoni, kusababisha taharuki miongoni mwa wafanyabiashara, wakazi,

Aliiambia Anadolu kuwa mwenyekiti wa manispaa Vitalis Neji, kwa kushirikiana na maafisa wa usalama, wameenda eneo hilo kutuliza hali na kuzuai matukio mengine ya vurugu.

Mmoja wa walioshuhudia aliyefahamika kwa jina la Peter anasema washambuliaji walitokea katika mlima wa karibu na eneo hilo, na kuanza kufyatua risasi hewani kabla ya kuchoma baadhi ya maeneo ya soko.

Shambulio hilo linakuja siku mbili baada ya shambulio lingine katika eneo la Abande, pia lililoko katika Manispaa ya Kwande, na kuwaua watu wasiopungua 17, kudhihirisha hofu ya ukosefu wa usalama katika eneo hilo.

Wakazi wamekuwa wakitaka serikali ya jimbo na ile serikali kuu kuimarisha doria za usalama na kulinda jamii vyema kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara.