Utajiri wa Afrika: Jamii ya Turkana

JAmii ya Turkana wanaunda sehemu ya makabila ya Nilotic na wanachukuliwa kuwa jamii ya tatu kwa ukubwa wa wafugaji nchini Kenya, baada ya Wakalenjin na Wajaluo, wakiwa wengi zaidi kuliko Wamasai.

By Coletta Wanjohi
Jamii ya Turkana inapatikana Kenya / Reuters

Kila mwaka, Kenya huandaa Tamasha la utalii na kitamaduni la Kaunti ya Turkana linaitwa Tobong’u Lore.

Tamasha hili ambalo limezinduliwa na serikali ya Kaunti ya Turkana miaka iliyopita, kwa miaka mingi, limekuwa likifanyika kwa mafanikio makubwa kila mwaka.

Neno Tobong’u Lore linamaanisha ‘kuja nyumbani’ au ‘karibu nyumbani’ katika lugha ya Turkana, hutumika kama mpango wa jamii kusherehekea utamaduni, kuthamini utofauti na kuleta umoja na amani.

Tamasha hilo huchukua siku tatu hadi nne ambapo wenyeji na watalii huja na kujionea utajiri wa tamaduni ya Turkana.Katika tamasha hilo, kuna mambo ya kuvutia ambayo unapaswa kuyajua kuhusu tamasha la Tobong'u Lore.

Lakini Waturkana ni kina nani?

Kabila la Turkana linaishi katika wilaya ya Turkana katika Mkoa wa Bonde la Ufa nchini Kenya. Wanaunda sehemu ya makabila ya Nilotic na wanachukuliwa kuwa jamii ya tatu kwa ukubwa wa wafugaji nchini Kenya, baada ya Wakalenjin na Wajaluo, wakiwa wengi zaidi kuliko Wamasai.

Jamii zinazofanana na Waturkana wa Kenya wanaishi Uganda, Kenya, Sudan Kusini na Ethiopia.

Waturkana wanaaminika kuwa walitoka eneo la Karamojong kaskazini mashariki mwa Uganda.

Simulizi zinaonyesha kwamba walifika Kenya wakimkimbiza fahali asiyetii.Waturkana hawana makazi ya kudumu, mara kwa mara wanahamahama pindi vyanzo vya chakula na maji vikiisha.

Sawa na Wamasai na Wasamburu, Waturkana huvaa mavazi yenye rangi za kuvutia.Wanawake hujipamba kwa shanga za rangi nyangavu, na wanaume hupaka nywele zao kwa udongo wenye rangi maalum.

Msimamo wa kijamii wa mwanamke katika kabila hilo unadhihirika kwa wingi na mtindo wa mapambo anayovaa.

Kama tu Wamasai, maisha ya Waturkana yanategemea mifugo yao kutoa riziki - ingawa hawaheshimu mifugo kama ilivyo kwa jamii ya Wamasai.Waturkana hufuga ngamia kwa sababu kuu mbili.

Ya kwanza ni kwa matumizi yao kama mnyama anayestahamili hali ngumu ya mazingira ya jangwa. Ya pili ni kwa maziwa yao yenye lishe ambayo ni rahisi kuyeyushwa.

Maisha yao yanategemea mazao ya wanyama - kama vile maziwa, damu, ngozi na nyama. Pesa yoyote inayopatikana kutokana na mauzo ya mifugo hutumika kununua bidhaa kama vile mahindi, maharage, sukari, tumbaku na mbogamboga.

Waturkana wanaishi kama kitengo cha kijamii kinachoitwa awi - hii inajumuisha mwanamume, wake, watoto na wanawake wanaomtegemea.

Ukubwa wa awi hutofautiana kulingana na utajiri, lakini ya wastani ni takriban watu 20-25. Mkuu wa kaya 'anamiliki' mifugo, lakini imegawiwa kwa wanawake – idadi ya wanyama wanaopokelewa inategemea hali ya wanawake ndani ya awi.Tofauti na makabila mengine ya kuhamahama,

Waturkana hawana desturi nyingi tata au miundo thabiti ya kijamii. Kila familia ya Turkana ina mwelekeo wa kujitegemea, ingawa, wakati fulani, familia kadhaa zinaweza kulisha mifugo yao kwa pamoja