Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuwa makubaliano makubwa yamefikiwa na Iran ili kumaliza vita vya Mashariki ya Kati, akisema anatarajia mkataba huo kutiwa saini barani Ulaya katika siku chache zijazo.
"Tumefikia makubaliano makubwa kuhusu vita na Iran," Trump aliwaambia waandishi wa habari katika Ofisi ya Oval, akiongeza kuwa makubaliano hayo "yanasubiri kukamilishwa kwa nyaraka, jambo ambalo linapaswa kufanyika katika siku chache zijazo; huenda tukawa na hafla ya kutia saini, labda barani Ulaya."
Trump amsifu Erdogan wa Uturuki kwa kusaidia kumaliza vita kati ya Marekani na Iran
Rais Donald Trump amesema atazungumza na Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ambaye amesema alikuwa na mchango mkubwa katika kusaidia kufanikisha juhudi za upatanishi zilizosaidia kumaliza vita kati ya Marekani na Iran.
Israel imeshangazwa na uamuzi wa Trump wa kusitisha mashambulizi dhidi ya Iran
Israel imeshangazwa na tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump kwamba alikuwa amesitisha mashambulizi yaliyokuwa yamepangwa dhidi ya Iran, huku Israel ikidaiwa kutokuwa na taarifa kuhusu makubaliano yoyote ya karibu kati ya Iran na Marekani, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Israel na CNN.
Kituo cha habari cha Channel 12 kiliripoti kuwa maafisa wa Israel walikumbwa na mshangao kufuatia ujumbe uliowekwa na Trump kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social.
Kulingana na kituo hicho, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alipewa taarifa kuhusu tangazo la Trump alipokuwa akihudhuria kikao cha Baraza la Mawaziri.


















