Ndege iliyobeba msaada wa chakula yaanguka Sudan Kusini, watatu wafariki

Ndege iliyokuwa ikisafirisha msaada wa chakula kwa shirika la kimataifa la Samaritan Purse ilianguka katika Jimbo la Unity nchini Sudan Kusini siku ya Jumanne, wafanyakazi wake wote watatu wamefariki, afisa wa shirika hilo amesema.

By
Ndege hiyo ilianguka takribani kilomita 20 kutoka Uwanja wa Ndege wa Leer, katika kaunti ya Leer. /

Ndege hiyo, iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni ya Nari Air, ilikuwa inasafirisha tani 2 za misaada kutoka mji mkuu, Juba, kuwapelekea watu waliolazimika kuhama makazi yao kutokana na mafuriko, kwa mujibu wa naibu mkurugenzi wa shirika la Samaritan Purse nchini Sudan Kusini, Bikram Rai, alipozungumza na shirika la habari la Reuters.

“Timu yetu imefika eneo la ajali, na kwa huzuni kubwa ninathibitisha kwamba wafanyakazi wote watatu wamefariki dunia,” Rai alisema.

Ndege hiyo ilianguka takribani kilomita 20 kutoka Uwanja wa Ndege wa Leer, katika kaunti ya Leer, jimbo lenye utajiri wa mafuta la Unity, karibu na mpaka wa Sudan, majira ya saa 2 asubuhi (0600 GMT).

shirika la ndege la Nari Air halikutoa ufafanuzi wowote hadi sasa. Hakukuwa na taarifa kuhusu aina au modeli ya ndege hiyo.

Kwenye tovuti yake, Nari Air inasema inafanya shughuli zake nchini Sudan Kusini na inatoa huduma mbalimbali ikiwemo usafiri wa kukodi kwa mizigo na abiria.