Takriban thuluthi mbili ya wavutaji sigara nchini Uturuki wanaanza kutumia tumbaku kabla ya umri wa miaka 18, huku magonjwa yanayohusiana na tumbaku yakisababisha takriban vifo 100,000 kila mwaka, hivyo kuonesha umuhimu wa kuchukuliwa hatua za haraka.
Wataalamu wa afya wanatahadharisha kwamba umri wa vijana ndio mbaya zaidi wa kuwa na tabia za uraibu kutokana na sababu kadhaa ikiwemo makundi, ushawishi kutoka mitandao ya kijamii, na taarifa potofu kuhusu afya na madhara na upatikanaji rahisi wa bidhaa za nikotini.
Maatumizi ya nikotini katika umri mdogo au ujana yanaweza kuwa na madhara katika ukuaji wa ubongo, hivyo kusababisha matatizo ya muda mrefu.
Matumizi ya tumbaku katika umri mdogo pia yanaweza kusababisha matumizi ya uraibu wa ulevi katika maisha ya baadae.
Kliniki za Wizara ya Afya za kuzuia uvutaji sigara kwa vijana zinalenga kutoa tathmini kwa vijana, ushauri nasaha na matibabu.
Kliniki pia zinatoa msaada wa ushuhuda kwa kuwashirikisha wanasaikolojia wa watoto na vijana, watumishi wa jamii na wabobezi wengine inapolazimika.
Maafisa wa afya wanasema hatua za awali ni muhimu sio tu kwa kuzuia matumizi ya tumbaku bali pia kuzuia utegemezi wa nikotini kuwa uraibu wa muda mrefu na kupunguza athari zake kiafya.
Upanuzi wa kliniki nchi nzima
Kliniki mpya zimeanza kufanya kazi Juni 2026 na hivi sasa zinatoa huduma katika vituo saba katika maeneo ya Agri, Ankara, Bursa, Canakkale, Corum na Kutahya.
Wizara ina mpango wa kupanua mpango huo nchi nzima kwa kuongeza idadi ya vituo na mwishowe kufanya huduma za vijana za kuacha uvutaji sigara kupatinana katika kila mkoa.
Uturuki hivi sasa ina kliniki 1,600 zinazohudumia watu nchi nzima kuanzia Julai 9, 2026.
Wizara pia imeandaa muongozo wa kliniki kwa wataalamu wanaofanya kazi katika vituo vipya.



















