| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Gwiji wa saratanji Judit Polgar ‘aukataa’ Urais wa Hungaria
Polgar, ambaye alitimiza miaka 50, Alhamisi iliyopita, alikuwa ni bingwa wa mchezo wa saratanji kwa miaka 25, kabla ya kustaafu mwaka 2014.
Gwiji wa saratanji Judit Polgar ‘aukataa’ Urais wa Hungaria
Polgar, ambaye alitimiza miaka 50, Alhamisi iliyopita, alikuwa ni bingwa wa mchezo wa saratanji kwa miaka 25, kabla ya kustaafu mwaka 2014.

Gwiji wa mchezo wa saratanji kutoka Hungaria, Judit Polgar amekataa ofa kutoka kwa Waziri Mkuu Peter Magyar, ya kushika hatamu ya uongozi wa nchi hiyo, badala ya Viktor Orban.

"Sidhani kama nina nguvu ya kuliunganisha taifa lililogawanyika, siku tayari kwa hilo," alisema Polgar kupitia mitandao ya kijamii.

"Nitafanya kadiri ya uwezo wangu kumuunga mkono rais ajaye ili aweze kutimiza malengo yake," aliongeza.

Polgar, ambaye alitimiza miaka 50, Alhamisi iliyopita, alikuwa ni bingwa wa mchezo wa saratanji kwa miaka 25, kabla ya kustaafu mwaka 2014.

Licha ya umaarufu na heshima yake nchini Hungaria, Polgar amegoma kujihusisha na chama chochote cha kisiasa nchini humo.

CHANZO:AFP