Jumla ya tani 30 za misaada ya kibinadamu kutoka Uturuki zimewasili nchini Venezuela kufuatia tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo.
Msaada huo ulipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Simon Bolivar na balozi wa Uturuki nchini humoi, Naci Aydan Karamanoglu, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela, Yvan Gil.
Akizungumza baada ya kupokea misaada hiyo, Karamanoglu alisema taasisi za Uturuki zimefanya jitihada kubwa mara baada ya kutokea kwa janga hilo nchini Venezuela, ikiwemo kusaidia juhudi za uokoaji.
"Mamlaka za Venezuela zimepongeza jitihada zetu. Hivyo basi, ningependa kushukuru Majeshi ya Ulinzi ya Uturuki pamoja na taasisi zingine," alisema.
Kulingana na Karamanoglu, Venezuela ilituma vikosi vya uokoaji, mara baada ya Uturuki kukumbwa na tetemeko la ardhi Februari 6, 2023.
"Walijitolea kwa hali na mali katika kutusaidia,” alieleza.
Misaada hiyo ni pamoja na mahema 275 yaliyotolewa na shirika la AFAD na tani 7 za madawa mbalimbali.
"Tutaendelea kutoa msaada na Uturuki itaendelea kuwa karibu na watu wa Venezuela," aliongeza Karamanoglu.
Kwa upande wake, Gil aliishuruku Uturuki kwa msaada wake, akisema kuwa una maana kubwa wa raia wa Venezuela.
"Kwa niaba ya Kaimu Rais Delcy Rodriguez, tungependa kumshukuru Rais Recep Tayyip Erdogan, serikali ya Uturuki na watu wa nchi hiyo, pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan, ambaye bado tunaendelea kuwasiliana toka kutokea kwa tukio hilo,” alisema.























