| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Rais Donald Trump ataka ahusishwe uteuzi wa kiongozi mpya wa Iran
Akizungumza siku ya Alhamisi, Trump amesema kuwa Mojtaba Khamenei, mtoto wa Khamenei aliyependekezwa kumrithi baba yake, hana uwezo wa kuiongoza Iran.
Rais Donald Trump ataka ahusishwe uteuzi wa kiongozi mpya wa Iran
Rais Donald Trump wa Marekani./Picha:Wengine
5 Machi 2026

Rais wa Marekani Donald Trump amesisitiza kuwa anapaswa kuhusishwa kwenye kumchagua mtu anayefaa kuiongoza Iran kwa sasa, kufuatia kifo cha Ayatollah Ali Khamenei.

Akizungumza siku ya Alhamisi, Trump amesema kuwa Mojtaba Khamenei, mtoto wa Khamenei aliyependekezwa kumrithi baba yake, hana uwezo wa kuiongoza Iran.

"Mojtaba Khamenei hana uwezo wa kuiongoza Iran. Natakiwa nihusishwe kwenye uteuzi wa kiongozi mpya wa Iran, kama ilivyofanyika kwa Delcy wa Venezuela,” alisema Trump.

Kiongozi huyo wa Marekani alikuwa akitolea mfano wa rais wa mpito wa Venezuela, Delcy Rodriguez ambaye alishirikiana na Rais Trump, baada ya kuondolewa kwa Nicolas Maduro.

"Simkubali mtoto wa Khamenei kabisa. Tunataka mtu ambaye ataleta amani na maelewano nchini Iran,” alisema Trump katika mahojiano yake na chombo cha habari cha Axios.

CHANZO:AFP