| Swahili
MICHEZO
1 dk kusoma
Trump aionya FIFA kuhusu kumtimua Gianni Infantino
Rais wa Marekani anasema Shirikisho hilo la Soka Duniani litakuwa linafanya 'makosa makubwa' iwapo litajaribu hilo
Trump aionya FIFA kuhusu kumtimua Gianni Infantino
Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa FIFA Gianni Infantino.

Rais wa Marekani Donald Trump ameonya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kuhusu kumuondoa rais wa FIFA, Gianni Infantino, akisema shirikisho hilo litakuwa linafanya “makosa makubwa” iwapo litajaribu hilo.

“FIFA itakuwa inafanya makosa makubwa ikiwa, kwa sababu zozote zile, wafkirie kumuondoa Rais Gianni Infantino,” Trump alisema siku ya Jumatatu katika ujumbe kwenye akaunti ya mtandao wa kijamii wa Truth Social.

Trump alimpongeza Infantino akisema “mtu mahiri,” akieleza kuwa amesimamia “Kombe la Dunia lenye mafanikio makubwa zaidi.”

“Akiondoka, haitopata mafanikio au kupata faida kubwa tena!” alisema.

Infantino amekabiliana na shinikizo kutokana na mpango wake uliotibuka wa kutaka kuuza hisa za Kombe la Dunia kwa wawekezaji binafsi.

Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA), Mashirikisho ya Soka ya Marekani ya Kaskazini, Marekani ya Kati na lile la Karibi (CONCACAF) pamoja na Shirikisho la Bara Asia (AFC) yalisema kwenye barua ya wazi siku ya Jumatatu kuwa mpango huo "ni kinyume na imani" kwa yale ambayo taasisi za FIFA zinatakiwa kutimiza, yakionya kuwa "wakati imani inapotoweka kwa kuhadaiwa, wakati mtu mmoja anapojiwekea majukumu na mamlaka binafsi, jukumu la msingi limetelekezwa."

FIFA iliomba radhi wiki iliopita kwa makosa yaliyoyotokea kuhusu mpango huo, akisema maafisa waandamizi katika mkutano nchini Morocco "walithibitisha kuunga mkono kikamilifu" urais wa Infantino.

CHANZO:َAA