Shirika la ndege la Uturuki limesema kuwa litarejesha safari zake za Damascus, Beirut na Amman, mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu.
Kupitia taarifa iliyowekwa kwenye tovuti yake, Turkish Airlines ilisema kuwa safari hizo zitarejea, ifikapo Mei 1.
Safari za ndege kuelekea Mashariki ya Kati zilisitishwa kuanzia Februari 28 kutokana na hofu ya usalama wa anga.
CHANZO:AA
















