| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Virusi vya Hanta vyaua 3 nchini Venezuela
Hantavirus ni aina ya virusi vinavyopatikana kwenye wanyama wagugunaji kama panya, na mara nyingi binadamu huambukizwa virusi hivyo kwa kupumua hewa inayotokana na kinyesi cha panya kilichokauka.
Virusi vya Hanta vyaua 3 nchini Venezuela
Hantavirus ni aina ya virusi vinavyopatikana kwenye wanyama wagugunaji kama panya./Picha:Others

Watu wapatao watatu wamefariki dunia baada ya kuambukizwa ugonjwa wa virusi vya Hanta, kulingana na Wizara ya Afya ya nchi hiyo.

Taarifa kutoka wizara hiyo, ilidai kuwa watu hao walipoteza maisha katika eneo la kaskazinimashariki la Venezuela, linalojulikana kama Anzoategui.

Hata hivyo, wizara hiyo iliondoa uwezekano wa watu hao kuwa wameambukizwa kwa njia ya binadamu.

Wizara hiyo, pia ilitupilia mbali madai kuwa, watu hao kuhusishwa na vifo vya wahudumu wawili wa afya katika eneo la  Barinas.

"Hakuna uhusiano wowote na vifo vyao," wizara hiyo ilisisitiza.

Hantavirus ni aina ya virusi vinavyopatikana kwenye wanyama wagugunaji kama panya, na mara nyingi binadamu huambukizwa virusi hivyo kwa kupumua hewa inayotokana na kinyesi cha panya kilichokauka.

Kwa mara ya kwanza, ugonjwa huo uliripotiwa kutokea katika meli ya kitalii ya MV Hondius, mwezi Aprili mwaka huu, na kuua watu watatu ndani ya meli hiyo.

Hata hivyo, kufikia mwanzoni mwa mwezi Julai, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kumalizika kwa ugonjwa huo.

CHANZO:AFP