Serikali ya Burundi imeanza mchakato wa kuwaondoa wanajeshi wake nchini Somalia kutokana na mizozo ya ugawaji wa idadi ya askari katika ujumbe mpya wa Umoja wa Afrika (AUSSOM).
Burundi imetangaza rasmi mpango huo, ikiwa ni sanjari na nchi nyingine kama Uganda ambayo pia imeanza mchakato wa kuondoa wanajeshi wake baada ya miaka mingi ya huduma ya ulinzi wa amani.
ZILIZOPENDEKEZWA
Uamuzi huu umezua maswali na wasiwasi kuhusu mustakabali wa usalama wa Somalia, uthabiti wa kikosi cha Umoja wa Afrika (AUSSOM), na jinsi mapambano dhidi ya kundi la Al-Shabaab yatakavyoendelea bila uwepo wa vikosi hivyo.
CHANZO:TRT Afrika Swahili




















