| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Mawaziri wa bara Arabu, Waislamu wakutana Jordan kujadili kwa pamoja Jerusalem Mashariki inayokaliwa
Wanadiplomasia waandamizi wanakutana mjini Amman kujadili hatua ya pamoja ya kile wanachokitaja kuwa mashambulizi ya Israel yanayolenga kufuta urithi wa Jerusalem Mashariki na maeneo matakatifu ya Kiislamu na Kikristo.
Mawaziri wa bara Arabu, Waislamu wakutana Jordan kujadili kwa pamoja Jerusalem Mashariki inayokaliwa
Mawaziri wa mambo ya bara Arabu, na mataifa ya Kiislamu wanahudhuria mkutano mjini Amman, Jordan Agosti 5 2026. (Reuters)

Mawaziri wa mambo ya nje wa bara Arabu na mataifa ya Kiislamu wanakutana nchini Jordan siku ya Jumatano kwa lengo la kuwa na msimamo mmoja kuhusu Jerusalem Mashariki huku kukiwa na wasiwasi kuhusu hatua ya Israel katika miji inayokaliwa na miji maeneo matukufu.

Mkutano huo mjini Amman umewaleta pamoja wajumbe wa kamati ya mawaziri wa bara Arabu kuhusu Jerusalem Mashariki, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Waarabu wa Ahmed Aboul Gheit, na mawaziri wa mambo ya nje wa Uturuki, Pakistan, Indonesia na Malaysia, kulingana na shirika la habari la Jordan Petra.

Mawaziri hao walijadili yanayojiri hivi karibuni katika eneo la Jerusalem Mashariki linalokaliwa na juhudi za kuwa na msimamo wa pamoja wa kidiplomasia kwa kile walichoeleza kuwa ni sera za Israel zinazoathiri urithi wa mji huo, urithi wa kidini na historia.

Fidan afanya mazungumzo ya mataifa mawili

Pembeni mwa mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan alifanya mazungumzo ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Ayman Safadi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria Ahmed Attaf, Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ilisema.

Jordan ilikuwa mwenyeji wa mkutano huo ikiwa katika nafasi yake kama mlezi wa maeneo takatifu ya Waislamu na Wakristo Jerusalem Mashariki.

Kamati ya mawaziri wa bara Arabu inajumuisha Jordan, Tunisia, Algeria, Saudi Arabia, Somalia, Iraq, Qatar, Misri na Morocco, pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Waarabu.

Mkutano huo unakuja huku kukiwa hatua za Israel ambazo mataifa ya Kiarabu na Kiislamu yanasema yanatishia hadhi na hali ya eneo linalokaliwa na Jerusalem Masahriki na sehemu takatifu.

CHANZO:TRT World and Agencies
Soma zaidi
Zaidi ya watu 4,500 wamekimbia makazi yao Darfur na Blue Nile nchini Sudan: UN
Israel yaagiza kufungwa kwa ubalozi wa Uingereza Jerusalem Mashariki inayokaliwa ndani ya siku 30
Uingereza na Ufaransa ni miongoni mwa nchi 12 zinazopanga kusitisha biashara na walowezi wa Israel
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu yatoa wito wa kulindwa kwa Wapalestina, yapinga kuondolewa kwa lazima
Iran yaonya Korea Kusini dhidi ya kutuma vikosi vya kijeshi katika Mlango-Bahari wa Hormuz
Qatar: Nchi za Ghuba haziwezi kutegemea Marekani pekee kulinda usalama wao
Iran yafanya 'mashambulizi ya kulipiza kisasi' baada ya Marekani kushambulia meli za mafuta
Futeni madeni yao, watumeni kuivamia Iran: Gazeti la Israel lapendekeza mpango kwa Wamarekani
Urusi, Ukraine washambuliana kwa droni huku makao makuu ya usalama Ukraine yakilengwa
Watu kadhaa wameuawa katika mapigano kati ya Wahouthi na vikosi vya Serikali nchini Yemen
Trump: Marekani inapigana na Iran kulinda washirika wake
Netanyahu awalaumu wakuu wa usalama kwa kukosa kumuamsha Oktoba 7
Iran yawataka raia wake kupunguza matumizi ya petroli
Marekani yashambulia Kisiwa cha Iran, watu kadhaa wauawa na kujeruhiwa
Mbu aliyeletwa na ndege Ujerumani asababisha vifo vya watu wawili
Trump: Putin hataishambulia nchi yoyote iliyoko ndani ya NATO
Rais wa Iran atoa wito kwa nchi za Kiislamu kutoruhusu mashambulizi kutoka kwao
Wanaolenga kuyumbisha eneo letu watashindwa: Rais Erdogan wa Uturuki
Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema Iran “inaporomoka kabisa”
Iran yazitahadharisha nchi jirani dhidi ya kujiunga na 'vita vya kiuchumi' vya Marekani