| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Bidhaa za Uturuki kupata alama ya Umoja wa Ulaya
Mpango huo unalenga kuunga mkono uzalishaji wa bidhaa ndani ya Umoja wa Ulaya na kupambana na ushindani usiokuwa na uwiano.
Bidhaa za Uturuki kupata alama ya Umoja wa Ulaya
Umoja wa Ulaya na Uturuki./Picha:AP

Tume ya Umoja wa Ulaya imesema kuwa bidhaa Uturuki zitawekewa nembo ya umoja huo, chini ya mkakati wa viwanda wa wenye kutoa fursa ya ruzuku.

Hatua hiyo, inadhihirisha utayari wa Umoja wa Ulaya wa kufanya biashara kwa ukaribu na Uturuki.

Maofisa wanasema kuwa, mpango huo unalenga kuunga mkono uzalishaji wa bidhaa ndani ya Umoja wa Ulaya na kupambana na ushindani usiokuwa na uwiano.

Viwanda mbalimbali barani Ulaya, hususani kwenye sekta ya teknolojia, ujenzi na kadhalika, vimekumbana na hali kama hiyo kutoka kwa wazalishaji wa kichina.

Kupitia mkakati huo, Umoja wa Ulaya unalenga kutumia mikakati ya manunuzi ya umma, ruzuku na zabuni ili kuongeza mahijati ya bidhaa za kimkakati zilizotengenezwa Ulaya.

Umoja wa Ulaya kuimarisha biashara ya magari ya Uturuki

Umoja wa Ulaya na Uturuki zinakutana katika Ushuru wa Forodha, huku mpango huo ukitoa ufafanuzi na uhakika kwa makampuni ya Kituruki yaliyo Ulaya pamoja na bidhaa wanazozalisha.

Hata hivyo, kwa sasa makampuni ya Uturuki hayatokuwa na uwezo wa kushiriki moja kwa moja kwenye zabuni ndani ya Umoja wa Ulaya, ikiwemo ujenzi wa shule, hospitali, kulingana na Msemaji wa Tume ya Umoja wa Ulaya.

Licha ya hayo, bidhaa mbalimbali kama vile saruji na mabati zinunuliwazo na makampuni ya Ulaya kutoka Uturuki, bado zinaweza kutumika katika miradi yenye kufadhiliwa kupitia miradi ya manunuzi ya Umoja wa Ulaya.

“Kwa sasa, Uturuki itapata hadhi sawa kama ilivyo kwa wanachama wengine wa Umoja wa Ulaya,” alisema msemaji huyo.

Soma zaidi
Uturuki yapiga marufuku mitandao kwa watoto chini ya miaka 15, mabadiliko makubwa ya kidijitali
Hakuna upungufu wa mafuta ya ndege nchini Uturuki: waziri
Wachambuzi wanaonya EU dhidi ya kujitenga na Uturuki huku kukiwa na changamoto za kiusalama
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Fidan kufanya ziara rasmi ya siku mbili nchini Uingereza
Tamasha kubwa la sayansi kwa vijana barani Afrika limefanyika Côte d'Ivoire
Uturuki inakataa ramani za bahari za Ugiriki ikisema kuwa zinakiuka sheria za kimataifa
COP31 huko Antalya kuanzisha enzi mpya ya ushirikiano wa hali ya hewa: Waziri Kurum wa Uturuki
Ishara ya Uganda katika Jukwaa la Diplomasia la Antalya inaonyesha kujitolea kwa uhusiano wa Uturuki
Viwanda vya ujenzi wa meli vya Uturuki katika maonyesho ya US Sea-Air-Space 2026
Uturuki imepongeza uteuzi wa gavana mwenye asili ya Turkmeni katika mkoa wa Kirkuk, Iraq
Erdogan afanya mazungumzo na viongozi wa Burundi, Libya kando ya Jukwaa la Diplomasia la Antalya
Waziri Mkuu wa Pakistan Sharif anaondoka Antalya na sifa kwa Rais Erdogan, kushinikiza uhusiano
Mke wa rais wa Uturuki ahudhuria jopo la 'Moyo Mmoja kwa Palestina' katika Kongamano la Antalya
Rais Erdogan akutana na viongozi wa Slovenia, Comoro, DRC katika Jukwaa la Diplomasia la Antalya
Israel inatumia usalama kama kisingizio cha kunyakua  'ardhi zaidi': Waziri Fidan
Fidan wa Uturuki akutana na mawaziri w mambo ya nje wa Misri, Pakistan na Saudi Arabia
Erdogan aonya kuhusu migogoro ya dunia, ataka diplomasia, utulivu wa kikanda
Viongozi mbalimbali wahudhuria Jukwaa la Kidiplomasia la Antalya
Spika wa Bunge la Uturuki ataka Israel iondolewe Umoja wa Mataifa
Erdogan atuma salamu za rambirambi kufuatia shambulio la risasi shuleni katika jimbo la kusini