Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda imesema kuwa wanafunzi 43 wa Uganda waliokuwa nchini Iran wakati wa uvamizi wa Marekani na Israel dhidi ya nchi hiyo mwishoni mwa juma, walihamishwa hadi Uturuki na sasa wanasafirishwa kwa ndege kurejea nyumbani.
Wanatarajiwa kuwasili Uganda Machi 5, 2026.
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Vincent Bagiire, alipokuwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, kujibu hoja za ukaguzi katika ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Wanafunzi hao walihamishwa kutoka mji mkuu wa Iran, Tehran kwa kutumia usafiri wa mabasi katika safari ndefu ya saa 24 hadi mpaka wa Gurbulak wa Uturuki na Iran.
Uganda imeishukuru serikali ya Uturuki kwa kuwapa viza raia wake ili waweze kuunganisha safari ya kurudi nyumbani.
















