| Swahili
MICHEZO
1 dk kusoma
Manchester City yasuwasuwa katika kusaka ubingwa
Timu ya Pep Guardiola ya Manchester City imeteteleka katika kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kutoka sare ya 2-2 na Nottingham Forest.
Manchester City yasuwasuwa katika kusaka ubingwa
Mechi kati ya Manchester City na Nottingham Forest. /Reuters
5 Machi 2026

Manchester City ilianza vizuri kwenye mechi hiyo na kuapata magoli mawili kupitia Antoine Semenyo na Rodri dhidi ya Nottingham Forest ambao kwenye ati ati ya kushuka daraj. Matokeo haya yamewaacha kuwa nyumba ya wanaoongoza msimamo wa ligi Arsenal kwa alama saba.

Vijana wa Guardiola bado wana mechi moja mkononi dhidi ya Crystal Palace, lakini huenda pia ikawa fursa ya kuwapa wigo zaidi wachezaji wa Mikel Arteta.

City ilimiliki mpira kwa asilimia 70% na kushambulia mara 21 lakini uwezo wao wa kumiliki zaidi hadi mwisho ungetoa muelekeo wa mambo yatakavyokuwa mwezi Mei, kwa kuwa tayari sasa wamepoteza alama 13 kuanzia mwanzo wa msimu hadi sasa.

"Mambo ni mengi lakini kuna mechi ambazo hatukutarajia matokeo yake, kwa ujumla, tumecheza vizuri kwa dakika 90," alisema Guardiola. "Lazima ubadilishe mifumo, mipira ya mbali lazima ulinde eneo lako, lakini siyo kuhusu hatua hii au hatua nyingine, kwa ujumla mechi ilikuwa nzuri.

"Tulikuwa na nafasi nyingi dhidi ya timu ambayo ilijipanga kulinda zaidi, timu nzuri sana, [ambayo] ina ubunifu."

CHANZO:TRT Afrika Swahili