| Swahili
MICHEZO
2 dk kusoma
Gobena avunja rekodi ya Sydney Marathon huku Ethiopia ikitawala mbio za wanaume
Ramakongoana wa Lesotho ashtukiza kwa kunyakua nafasi ya tatu kutoka kwa Alphonse Simbu wa Tanzania aliyeishia nafasi ya nne.
Gobena avunja rekodi ya Sydney Marathon huku Ethiopia ikitawala mbio za wanaume
Muda wa ushindi wa Gobena ulifuta rekodi ya awali ya Sydney ya saa 2:06:06, iliyowekwa na mwanariadha mwenzake Hailemaryam Kiros mwaka 2025 / TRT Afrika Swahili

Addisu Gobena wa Ethiopia ameshinda mbio za Sydney Marathon kwa wanaume kwa muda wa saa 2:04:42, muda ambao ni rekodi mpya ya njia hiyo, akiboresha sana matokeo yake ya kushika nafasi ya pili katika mbio za mwaka jana.

Gobena alionyesha kiwango cha juu na kumaliza mbio hizo akiwa mbele kwa sekunde nne pekee dhidi ya M-Ethiopia mwenzake, Chimdessa Debele Gudeta, aliyemaliza kwa muda wa saa 2:04:46.

Tebello Ramakongoana wa Lesotho alishika nafasi ya tatu kwa muda wa saa 2:04:57 na kuleta matokeo ya kushtukiza, huku wanariadha wote watatu wakimaliza mbio hizo kwa muda bora zaidi kuliko rekodi ya awali ya njia hiyo.

Muda wa ushindi wa Gobena ulifuta rekodi ya awali ya Sydney ya saa 2:06:06, iliyowekwa na mwanariadha Muethiopia mwenzake Hailemaryam Kiros mwaka 2025, na kumfanya kuwa mwanariadha wa kiume wa mbio ndefu (marathon) mwenye kasi zaidi kuwahi kurekodiwa nchini Australia.

Simbu apokonywa nyama mdomoni

Matokeo haya yanaashiria maendeleo makubwa kwa Gobena, ambaye alirejea Sydney baada ya kushika nafasi ya pili mwaka jana. Sasa anaondoka katika jiji hilo la Australia akiwa na zawadi kubwa zaidi katika taaluma yake, ushindi katika mojawapo ya mbio kuu za dunia (World Marathon Majors) na rekodi mpya ya njia hiyo.

Alphonse Simbu wa Tanzania alirekodi muda sawa na Ramakongoana, akimaliza wa nne baada ya wawili hao kutenganishwa kwenye mstari wa kumalizia.

Muda wa saa 2:04:57 ulikuwa kiwango kizuri kwa Simbu katika ushiriki wake wa kwanza kwenye Sydney Marathon, akishindana na kundi la wanariadha waliokuwa na rekodi binafsi za muda wa chini ya saa 2:05.

Mwanariadha huyo wa Tanzania aliingia kwenye mbio hizo akiwa bingwa mtetezi wa dunia baada ya kuweka historia kwa kushinda mbio za marathon katika Mashindano ya Dunia ya Riadha ya mwaka 2025 jijini Tokyo.

Afrika Mashariki ilitawala mbio hizo za wanaume kwa kuchukua nafasi 16 kati ya 20 za juu. Ethiopia ilikuwa na wanariadha 10, Kenya ilikuwa na wanariadha 5, huku Tanzania ikiwakilishwa na mwanariadha mmoja. Hakukuwa na mshiriki kutoka Uganda.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Soma zaidi
Guye na Tigst waongoza Ethiopia kufagia mbio za Berlin Marathon
Mo Salah hatacheza mechi ya kufuzu AFCON dhidi ya Sudan Kusini kutokana na nyasi bandia za Uwanjani
Mechi za kuwania kufuzu AFCON 2027 zinaanza huku kukiwa na utata kuhusu bingwa mtetezi
Agnes Ng’etich aweka rekodi mpya ya dunia katika mbio za nusu marathoni za wanawake pekee
Mkuu wa shirikisho la Afrika aunga mkono Tanzania, Kenya na Uganda kuandaa AFCON 2027
Kenya kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Riadha ya Dunia 2029 ikiwa ya kwanza barani Afrika
FIFA yakanusha madai ya Morocco ya 'uwenyeji' wa mechi ya fainali ya Kombe la Dunia 2030
Erdogan akutana na timu ya Voliboli ya wanawake ya Uturuki baada ya ubingwa wa Ulaya
Timu ya wasichana ya Tanzania ya chini ya umri wa miaka 15 imetwaa ubingwa wa CECAFA
Mshambuliaji Aubameyang astaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Gabon
Antonio Rüdiger astaafu kuichezea timu yake ya taifa
Jepchirchir anaongoza ushindi wa 1-2 kwa Kenya jijini Sydney
Fenerbahce yaifunga Lyon 2-1 kuiwezesha kurejea Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya misimu 17
Mkuu wa Shirikisho la UEFA hataki nafasi ya Infantino, anachotaka ni ajiuzulu
Bondia wa zamani bingwa wa dunia Zolani Tete auawa kwa kupigwa risasi nchini Afrika Kusini
Guinea yatangaza nia ya kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika
FIFA yawaadhibu wachezaji wa Argentina, yaitoza faini shirikisho kwa matukio ya Kombe la Dunia
Cristiano Ronaldo atangaza azma yake ya kustaafu soka
Algeria imefanikiwa kupata medali kwa mara ya kwanza katika mashindano ya WAFCON baada ya kuishinda
Afrika Magharibi ving’ang'anizi kwa mara ya kwanza kwa nafasi ya tatu WAFCON