| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Wahamiaji zaidi ya 1,000 waokolewa pwani ya Afrika magharibi ndani ya wiki moja, MSF inasema
Maelfu ya vijana wamekuwa wakijaribu kuvuka kwa kutumia njia hiyo ya hatari kwa muda mrefu wakiwa ndani ya mashua zilizojaa na maboti makuu kuu.
Wahamiaji zaidi ya 1,000 waokolewa pwani ya Afrika magharibi ndani ya wiki moja, MSF inasema
Wengi wao walikuwa wanatoka Senegal na Gambia, ingawa kulikuwa na wengine kutoka Mali, Guinea, Cote d’Ivoire na mataifa mengine.

Wahamiaji zaidi ya 1,000 wameokolewa katika kipindi cha wiki moja pwani ya Afrika magharibi wakati wakijaribu kuvuka bahari hatari kuelekea Ulaya, shirika la misaada la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limesema.

Watu 1,046 walikuwa wanasafiri ndani ya mashua saba, ambazo zote zilianzia safari yake nchini Gambia na walikuwa wanaelekea katika Visiwa vya Canary nchini Hispania, kabla ya kukwama baharini, MSF ilisema katika taarifa siku ya Jumatatu.

Baada ya kupatikana mwisho wa wiki ya mwezi Agosti, walifikishwa mjini Nouadhibou, Mauritania na miji ya Rosso na Dakar nchini Senegal.

Maelfu ya vijana wamekuwa wakijaribu kuvuka kwa kutumia njia hiyo ya hatari kwa muda mrefu wakiwa ndani ya mashua zilizojaa na maboti makuu kuu kufika Ulaya kupitia Visiwa vya Canary nchini Hispania.

Kukimbia umaskini

Wengi wao wanakimbia umaskini kwa kutumia njia za hatari na mashua kuu kuu kutokana na nchi za Ulaya kuweka masharti makali ya kupatikana kwa viza za kusafiria na kuimarisha ulinzi mipakani .

Waliookolewa walikuwa na matatizo mbali mbali ya kiafya, ikiwemo kiu, kupoteza fahamu, matatizo ya mifupa, uchovu, na ngozi, matatizo ya tumbo na kifua, MSF ilisema.

Miongoni mwa wahamiaji hao kulikuwa na wanawake 134, ikiwemo mmoja aliyekuwa mjamzito, pamoja na watoto 88, shirika hilo lilisema.

Wengi wao walikuwa wanatoka Senegal na Gambia, ingawa kulikuwa na wengine kutoka Mali, Guinea, Cote d’Ivoire na mataifa mengine.

CHANZO:TRT Afrika Swahili