| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Mlipuko wa gesi katika mgodi wa waua watu 38, kujeruhi wengine kadhaa
Wakazi wanasema walioathirika walikuwa chini kwenye mgodi ambapo mlipuko ulitokea Jumatano asubuhi.
Mlipuko wa gesi katika mgodi wa waua watu 38, kujeruhi wengine kadhaa
Kihistoria Jimbo la Plateau linafahamika kuwa sehemu ya migodi. / REUTERS
tokea masaa 3

Mlipuko wa gesi siku ya Jumatano umewaua wachimba migodi wasiopungua 38 waliokuwa chini ya mgodi katika jimbo la kati la Nigeria la Plateau, vyanzo vya eneo hilo viliiambia AFP.

Watu wengine ishirini na saba walijeruhiwa katika mlipuko huo kwenye mgodi wa Kampanin Zurak wilaya ya Bashar jimbo la Plateau, kaimu kiongozi wa kijadi wa eneo hilo aliiambia AFP.

"Ni kweli kuwa kufikia sasa watu 38 wamethibitishwa kufariki na wengine kama 27 wamepelekwa hospitali," Alhaji Aliyu Adamu Idris amesema.

Ibrahim Dattijo Sani, mchimba migodi wa eneo la karibu na hapo, ameiambia AFP kuwa walioathirika walikuwa chini ya mgodi ambapo mlipuko ulitokea kati ya saa moja na nusu na saa mbili asubuhi.

"Tuko karibu na mgodi huo, watu walikuwa ndani mara ghafla tukasikia mlipuko wa gesi," Sani ameiambia AFP kwa njia ya simu.

Jimbo hilo linafahamika kuwa na migodi mengi, huku makao yake makuu ya Jos yakijulikana kama ‘‘Tin City’’. Lakini shughuli za uchimbaji zimepungua katika miaka ya hivi karibuni.

Nchi hiyo ya Afrika Magharibi imekuwa na ajali mbaya za migodini.

Watu wasiopungua 18 waliuawa katika jimbo la Zamfara kaskazini magharibi baada ya mwamba kusambaratika katika mgodi mmoja usio halai wakati mvua kubwa ziliponyesha mwezi Septemba.

CHANZO:TRT Afrika Swahili