| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Singapore: Wanyanyasaji mashuleni kukumbwa na adhabu ya viboko
Hata hivyo, makundi ya haki za kibinadamu yameshutumu uamuzi huo wa serikali ya nchi hiyo, licha ya serikali kusisitiza kuendelea nayo.
Singapore: Wanyanyasaji mashuleni kukumbwa na adhabu ya viboko
Uamuzi huo, ulijadiliwa bungeni siku ya Jumanne, huku wabunge wakitaka kufahamu uhusiano wa adhabu hiyo na unyanyasaji mashuleni./Picha:Wengine

Serikali ya Singapore imeanzisha kanuni mpya zenye kutoa adhabu ya viboko kwa wanaohusika na unyanyasaji wa wanafunzi wawapo mashuleni.

Hata hivyo, makundi ya haki za kibinadamu yameshutumu uamuzi huo wa serikali ya nchi hiyo, licha ya serikali kusisitiza kuendelea nayo.

Uamuzi huo, ulijadiliwa bungeni siku ya Jumanne, huku wabunge wakitaka kufahamu uhusiano wa adhabu hiyo na unyanyasaji mashuleni.

“Shule zetu zimeanza kutumia adhabu hii kutokana na ukubwa wa tatizo lenyewe," alisema Desmond Lee, Waziri wa Elimu wa nchi hiyo, siku ya Jumanne.

"Tutazingatia vigezo mbalimbali kama vile ukomavu wa mwanafunzi pia kufahamu kama adhabu ya viboko itawasaidia wanafunzi kujifunza kutokana na makosa yao."

Nchini Singapore, adhabu ya viboko ilirithishwa kutoka utawala wa kikoloni, licha wa Waingereza wenyewe kuitokomeza.

CHANZO:AFP