| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Rais wa Uturuki na Mwana Mfalme wa Saudia wajadili usalama wa kikanda na mpango wa amani wa Gaza
Rais wa Uturuki, Erdogan, amesema kuwa Uturuki imesikitishwa na mashambulizi yaliyolenga Saudi Arabia.
Rais wa Uturuki na Mwana Mfalme wa Saudia wajadili usalama wa kikanda na mpango wa amani wa Gaza
Erdogan amesema Uturuki imehuzunishwa na mashambulizi dhidi ya Saudi Arabia. / AA / AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Mwana wa Mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, viongozi hao wawili wamejadili masuala ya usalama wa kikanda, uhusiano wa mataifa yao mawili, pamoja na mpango wa amani wa Gaza, kwa mujibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na kurugenzi hiyo kwenye mtandao wa X siku ya Jumatatu, Erdogan amesema kuwa Uturuki imesikitishwa na mashambulizi yaliyolenga Saudi Arabia.

Aidha, amesisitiza kuwa Uturuki inaendelea kufanya juhudi za kufanikisha amani ya kudumu na kuhakikisha utulivu pamoja na usalama katika eneo lote.

Erdogan pia alieleza kuwa utekelezaji kamili wa hatua zilizowekwa katika awamu ya pili ya mpango wa amani wa Gaza na Israel ni muhimu kwa mafanikio ya mpango huo.

"Tunafuatilia kwa karibu yanayoendelea," Erdogan alisema, kwa mujibu wa taarifa hiyo.

CHANZO:AA