| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Mahakama yakataa ombi la Lissu kumuita Rais Samia kutoa ushahidi
Mahakama imekubali ombi la upande wa Utetezi la kuwaita viongozi watatu wa vyombo vya ulinzi na usalama kutoa ushahidi.
Mahakama yakataa ombi la Lissu kumuita Rais Samia kutoa ushahidi
Tundu Lissu aliomba Rais Samia, na viongozi wengine waitwe mahakamani kutoa ushahidi katika kesi hiyo. /

Mahakama Kuu, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imekataa ombi la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, la kuwaita Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine waandamizi wa Serikali kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili.

Lissu aliomba Rais Samia, Dkt. Philip Mpango, Kassim Majaliwa pamoja na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa waitwe mahakamani kutoa ushahidi katika kesi hiyo.

Hata hivyo, Mahakama imekubali ombi la upande wa Utetezi la kuwaita viongozi watatu wa vyombo vya ulinzi na usalama kutoa ushahidi.

Viongozi hao ni Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Camilius Wambura; Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jacob Mkunda; pamoja na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhani Kingai.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Dunstan Ndunguru akisaidiwa na Majaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.

Lissu anakabiliwa na shtaka la uhaini chini ya Kifungu cha 39(2)(d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu. Anadaiwa kuwa Aprili 3, 2025, alitoa kauli na kuchapisha ujumbe uliolenga kuhamasisha umma kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

CHANZO:TRT Afrika