Madagascar imetangaza hali ya dharura kote nchini kwa siku 15 Jumanne, ikieleza sababu kuwa ni kutatizwa kwa usambazaji nishati kutokana na vita vya Mashariki ya Kati, baraza lake la mawaziri limesema.
Serikali kadhaa za Afrika zilikabiliana na kuongezeka kwa bei za mafuta duniani, zilizochochewa na vita vya Iran, kwa wao kuongeza bei za mafuta, hatua za kuhifadhi nishati, au mgao wa umeme.
"Uamuzi huu umechukuliwa kufuatia tathmini kuwa nchi inakabiliwa na tatizo kubwa la usambazaji wa nishati kote kisiwani, kutokana na mapigano Mashariki ya Kati," baraza lilisema katika taarifa.
"Kutangaza hali ya dharura kunatoa muda kwa mamlaka kuchukuwa hatua za haraka ili kurudisha mifumo ya usambazaji wa nishati na kuhakikisha huduma za umma zinaendelea kutolewa."
Vyombo vya habari nchini Madagascar vilitangaza kuwepo kwa uhaba mkubwa wa mafuta kote nchini siku ya Jumanne.













