| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Kim Jong Un wa Korea Kaskazini asimamia mazoezi ya kijeshi
Kiongozi huyo alitumia fursa hiyo kuonesha vifaa vipya, vikiwemo vifaru vya kijeshi
Kim Jong Un wa Korea Kaskazini asimamia mazoezi ya kijeshi
Kwa mujibu wa chombo cha habari cha nchi hiyo, binti wa kiongozi huyo Ju-ae, pia alishiriki kwenye mazoezi hayo./Picha:Wengine
20 Machi 2026

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un amesimamia mazoezi ya kijeshi yaliyofanywa na jeshi la nchi hiyo.

Mazoezi hayo yamefanyika karibu na kambi ya jeshi jijini Pyongyang, kulingana na Shirika la Habari la Korea.

Mazoezi hayo yalihusisha maonesho ya vikosi maalumu na mifumo ya droni yenye kufanya upelelezi.

Kim alionesha kuridhishwa na mazorezi hayo, akisifia ufanisi wa vikosi vyake, hususani vile vya vifaru vya mashambulizi.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha nchi hiyo, binti wa kiongozi huyo Ju-ae, pia alishiriki kwenye mazoezi hayo.

CHANZO:AA