| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
WHO yaomba msaada wa ziada kukabiliana na mlipuko wa Ebola nchini DRC
Mlipuko wa Ebola, ambao unakuwa ni wa 17 kutokea katika historia ya nchi hiyo, ulianza kuripotiwa Mei 15, baada ya kutokea vifo kadhaa katika eneo la Ituri.
WHO yaomba msaada wa ziada kukabiliana na mlipuko wa Ebola nchini DRC
Mlipuko wa Ebola, ambao unakuwa ni wa 17 kutokea katika historia ya nchi hiyo ukiwa umeripotiwa Mei 15.

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limetoa wito wa kusaidiwa zaidi katika kukabiliana na ugonjwa wa nchini DRC.

"Ugonjwa huo unazidi kuenea na tunaelekea kuzidiwa uwezo wa kukabiliana na," alisema msemaji wa WHO, Tarik Jasarevic wakati akizungumza na wanahabari jijini Geneva.

Kulingana na Jasarevic, shirika hilo linahitaji fedha na msaada wa rasilimali ili kuongeza kasi ya kukabiliana na ugonjwa huo.

Kufikia sasa, jumla ya maambukizi 3,748 yamethibitishwa nchini DRC, vikiwemo vifo 1,657.

Jasarevic alisisitiza umuhimu wa kuongeza nguvu zaidi kwenye maeneo ambayo ugonjwa huo unaendelea kusambaa.

Mlipuko wa Ebola, ambao unatokea DRC kwa mara ya 17 sasa, ulianza kuripotiwa Mei 15, baada ya kutokea vifo kadhaa katika eneo la Ituri.

CHANZO:AFP