Mapinduzi ya Syria: 'Kiongozi dhalimu' anaanguka, wafungwa waachiliwa
Miaka sitini na moja ya utawala wa chama cha Baath cha Syria imemalizika.
Upinzani wa Syria ulitangaza katika taarifa yake kwa njia ya runinga kwamba umeikomboa Damascus na kuupindua utawala wa miaka 24 wa Bashar al Assad.
Upinzani ulisema "ulimng'oa 'dhalimu' Bashar al-Assad."
Wafungwa katika Gereza la Sednaya mjini Damascus, linalojulikana kwa ushirikiano wake na utawala na vitendo vya utesaji, waliachiliwa huru na waandamanaji waliovamia kituo hicho
Bashar al Assad wa Syria na familia yake wamekimbilia Urusi na wamepewa hifadhi na mamlaka ya Urusi.
Moscow inasema kuwa Assad na familia yake wamepewa hifadhi kwa misingi ya kibinadamu.
Israel inaendelea kushambulia kwa mabomu kusini na kati mwa Gaza
Israel ilishambulia kwa mabomu eneo la kati na kusini lililozingirwa Gaza, na kuua Wapalestina wanane na kujeruhi wengine kadhaa.
Mwanamume mmoja na mkewe waliuawa, na wengine sita, akiwemo binti yao mchanga, walijeruhiwa vibaya wakati shambulio la anga lilipopiga hema walimokuwa wakiishi katika mji wa Al-Zawayda katikati mwa Gaza.
Wapalestina sita zaidi waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati ndege isiyo na rubani ya Israel ilipolenga pikipiki na gari la kiraia katika eneo la Khirbat Al-Adas katika Jiji la Rafah.
Trump ahimiza mapatano ya haraka ya Ukraine, akidokeza uwezekano wa kujiondoa kwa NATO
Rais mteule wa Marekani Donald Trump ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano na mazungumzo kati ya Ukraine na Urusi ili kukomesha kile alichokiita "wendawazimu", na kumfanya Rais wa Ukraine Volodymr Zelenskyy na Kremlin kuorodhesha masharti yao.
Trump aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social kwamba Zelenskyy na Ukraine wangependa kufanya makubaliano na kuongeza kuwa Kiev imepoteza takriban wanajeshi 400,000.
Trump pia alisema katika mahojiano kwamba "atafikiria" kabisa kuondoka NATO ikiwa washirika "hawatalipa ada zao."
Trump amelalamika kwa muda mrefu kwamba serikali za Ulaya na Canada katika kambi ya ulinzi wa pande zote zinapakia bure matumizi ya kijeshi ya Marekani, mshirika mwenye nguvu zaidi katika NATO.
Na hatimaye…
Tanzania yaadhimisha miaka 63 ya Uhuru.
Tanzania bara inaadhimisha miaka 63 ya uhuru wake huku mikoa mbali mbali ikiandaa tamasha na hafla za sherehe hizo kwa maombi na maonyesho mengine ya kitamaduni.
Hata hivyo hii inafanyaika wakati Mama Samia Suluhu, Hassan, Rais wa Tanzania ametangaza kutofanywa sherehe zozote za kitaifa, huku akiagiza fedha zilizotengezwa sherehe hizo kutumika badala yake katika utoaji wa huduma za kijamii.
Kila Mkoa utajiandalia wenyewe sherehe zao.
