Watu 15 wamefariki na wengine 100 hawajulikani walipo baada ya maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa kufukia nyumba kadhaa katika vijiji vilivyopo mashariki mwa Uganda, ofisi ya Waziri Mkuu na polisi zilisema Alhamisi Novemba 28.
Maporomoko hayo yametokea siku ya Jumatano katika wilaya ya Bulambuli, takriban kilomita 300 mashariki mwa mji mkuu Kampala.
Takriban kaya 40 zilizikwa kabisa, Chama cha Msalaba Mwekundu cha Uganda kimesema takriban kaya 40 zimezikwa huku nyengine zikiharibiwa kwa kiasi.
Polisi imesema miundombinu ya barabara imeharibika hivyo kukwaza shughuli ya uokoaji..

00:21

00:21
Tazama Video zaidi
Maporomoko ya ardhi yauwa watu Uganda
Maafisa nchini Uganda wanasema maafa hayo yamesababisha vifo vya takriban watu 30 na kuharibu makumi ya nyumba katika mashariki mwa nchi.
Tazama Video zaidi