| Swahili
Maoni ya Watanzania kuhusu kulipa dhamana ya viza kuenda Marekani
02:15
Afrika
Maoni ya Watanzania kuhusu kulipa dhamana ya viza kuenda Marekani
Tanzania imekuwa ni nchi ya hivi karibuni kuingizwa katika orodha ya nchi ambazo raia wake wamewekewa masharti ya dhamana ya viza.

Kuanzia Oktoba 23, nchi hiyo ya Afrika Mashariki itakuwa katika kundi la nchi saba za Afrika, ambazo raia wake watatakiwa kulipa dhamana itakayorudishwa ya kati ya dola 5,000, sawa na shilingi milioni 12 za Tanzania au dola 15,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni 37.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, agizo hilo linawahusu wale watakaoomba viza kwa ajili ya biashara B-1 (Business) na utalii B-2 (Tourism).

Serikali ya Marekani imesema agizo hilo linafuatia taarifa za baadhi ya raia kutoka mataifa hayo kupitiliza muda wao pindi wanapokuwa nchini Marekani.

Hata hivyo, serikali ya Tanzania, imesema tayari imeingia katika mazungumzo na Marekani kuona ni jinsi gani nchi mbili hizo zinaweza kufikia muafaka wa kukabiliana na changamoto hiyo.

Miongoni mwa nchi hizo ni pamoja na Mali na Mauritania ambazo agizo hilo litaanza rasmi Oktoba 23, 2025.

Tazama Video zaidi
Magdalena Shauri : Dada anayepepea miongoni mwa vigogo wa riadha duniani
Gabriel Geay : Nyota wa riadha wa Tanzania 'Moto wa kuotea mbali'
Kiuno mkabaji Thomas Partey
Prince Harry ni Nani?
Mafao anayostahiki Nchimbi
John Welle: Kizazi kipya kinachopeperusha bendera ya Tanzania katika riadha
Kocha Yaya Toure
Ainua mkono wake juu kwa miaka 53 kuushusha chini
Edwin Watenya Sifuna ni nani?
Gerrard: Mwamba wa Liverpool