Sera ya faragha

TRT inalenga kuweka mazingira salama na ya kufurahisha kwa watumiaji wetu kwa kuweka taarifa zako binafsi kuwa siri unapotumia huduma za TRT. TRT imejitolea kuweka maelezo yako binafsi salama. Taarifa kama hizo zinapo tolewa, tunalazimika kisheria kutumia taarifa zako pamoja na sheria zote pamoja na Katiba ya Jamhuri ya Uturuki. Viungo vya Tovuti zingine tofauti na za TRT zina viungo vya tovuti vingine na vinaendeshwa na kampuni zingine. Kampuni hizi zingine zina sera zao za faragha ambazo tunakuhimiza ukague. TRT haiwajibiki na utendaji kazi wa faragha wa tovuti kama hizo za watu wengine na matumizi yako ya tovuti kama hizo ni kwa kuchukua tahadhari.

Unavyojiunga na huduma za TRT, taarifa zako binafsi kama vile jina lako, anwani ya barua pepe, anwani ya posta, simu au nambari ya simu ya mkononi au tarehe ya kuzaliwa zitaombwa kulingana na shughuli utakayofanya. Kwa kufanya hivyo unawezesha TRT kukupa ruhusa kufanya shughuli ulizochagua. Ukichagua kutotoa taarifa zako binafsi, baadhi ya huduma huenda zinaweza zisipatikane kwako.

TRT hukusanya taarifa zako binafsi ili kuunda jukwaa bora kwa watumiaji wetu. Maelezo yako binafsi hutusaidia kutoa huduma bora kwa wateja, kufanya utafiti na uchambuzi ili kuboresha maudhui, huduma na teknolojia yetu, na kuelekeza tovuti kule kwa watumiaji wetu.

TRT haigawi wala kusambaza taarifa zako binafsi na washirika wa nje, isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo katika sera hii ya faragha. Taarifa zako binafsi zinaweza kutumika miongoni mwa kikundi chetu cha ushirika ikiwa ni pamoja na vituo vingine vya TRT, na vitengo vingine vinavyoshirikiana na vituo vya TRT, wote ambao wanaweza kutumia maelezo yako kwa madhumuni yaliyotajwa katika sera hii ya faragha.

Iwapo ungependa kubadilisha maelezo yoyote yako binafsi ambayo tayari umetupatia, unaweza kutembelea taarifa za akaunti yako na kufanya mabadiliko ya chaguo lako.

Usalama wa taarifa zako binafsi ni muhimu sana kwetu, jambo ambalo hutufanya tujitahidi kuweka taarifa zako zote unazotupatia kwa siri. Programu za usalama zinaweza kutumika kuweka maelezo yako salama, hata hivyo hakuna njia ya utumaji kwenye mtandao au mbinu za usalama wa kielektroniki ambazo ni salama 100%, kwa hivyo hatuwezi kukuhakikishia usalama wake kamili.

Vidakuzi huundwa unapotumia tovuti kutembelea ukurasa mbalimbali mtandaoni kufuatilia mienendo yako/ Hii ni kwa ajili ya kukusaidia kuendelea pale ulipoishia, kukumbuka kuingia kwako kwa usajili, uteuzi wa mandhari, mapendeleo na vipengele vingine vya kuweka mapendeleo. Tovuti huhifadhi faili inayolingana (yenye kitambulisho sawa) na ile waliyoweka kwenye faili yako na katika faili hii wanaweza kufuatilia na kuweka taarifa za mienendo yako ndani ya tovuti na taarifa yoyote ambayo unaweza kuwa umetoa kwa hiari unapotembelea tovuti, kama vile barua pepe. Kwenye tovuti ya TRT, vidakuzi vitarekodi maelezo kuhusu mapendeleo yako ya mtandaoni na kuturuhusu kubadilisha tovuti zetu kulingana na mambo yanayokuvutia. Taarifa zinazotolewa na vidakuzi zinaweza kutusaidia kuchanganua wasifu wa wageni wetu na kutusaidia kukupa hali bora ya utumiaji. TRT hutumia maelezo haya kutoa huduma bora kwa watumiaji wake.

Unapopakua programu za TRT kwenye kifaa chochote, taarifa inaweza kufikiwa au kuhifadhiwa. Hii inatumika kwa njia sawa na kidakuzi cha ukurasa mtandaoni. ukurasa unachotembelea au kifaa pia kinaweza kuipa TRT taarifa kuhusu kifaa chako, kama vile kitambulisho cha kifaa au anwani ya IP.

TRT ina haki ya kurekebisha au kuboresha sera yake ya faragha wakati wowote. Ni wajibu wa watumiaji kuangalia kama sheria na masharti yamerekebishwa au kusahihishwa. Kwa hivyo, unakubali masharti yote ya matumizi yaliyowekwa hapa mradi tu uendelee kutumia lango za lugha zinazohusiana. Ikiwa hukubali masharti yaliyorekebishwa au yaliyoboreshwa tafadhali usitumie tovuti hii tena.