Leather tannery shop in Kano, Northern Nigeria/ AA

Miradi ya biashara midogo na mikubwa, maarufu kama SMEs – yanachukua sehemu kubwa ya makampuni ya sekta binafsi katika bara, na duniani kote kwa jumla.

Hao ndio wanaoendesha uchumi, wakizalisha ajira zaidi ya asilimia 80 katika bara la Afrika, na wachangiaji wakubwa wa pato la taifa katika nchi wanazofanya kazi.

Ni kutokana na hali hiyo, kwamba sio siri kukuwa kwa sekta binafsi kupitia makampuni madogo na ya kati, ni muhimu kwa ajira na ukuaji wa uchumi ambao Afrika unahitaji angalau kwa miaka kadhaa ijayo.

Vilevile mustakbali wa Afrika, unategemea kukuwa kwa mafanikio ya biashara, na kutokana na hilo, kutakuwa na uhakika wa maisha kwa idadi ya watu wanaoongezeka.

Bara la Afrika lina fursa nyingi za kibiashara, hii inatokana na kuwepo kwa soko la zaidi ya watu bilioni 1.2, lakini pia kukuwa kwa mafungamano ya kibiashara kutokana na kuendelezwa kwa maeneo huru ya biashara barani Afrika.

Kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa wanaofanya shughuli zao barani Africa, mazingira ya kufanya kazi yana changamoto, hasa kwa wale wanaotaka kujiendeleza.

Gharama za uendeshaji ni kubwa kutokana na miundombinu dhaifu iliyosababishwa na uwekezaji mdogo uliokuwa ukifanyika wa muda mrefu, ikiwemo mtandao wa usafari usiokuwa na uhakika, na uhaba wa upatikanaji wa nishati ya umeme. Pia kuna uhaba wa wafanyakazi wenye uzoefu wa masuala ya utawala wanaoweza kusaidia kukuza biashara.

Mtaji unahitajika kusaidia kukabiliana na baaadhi ya changamoto hizi na kufanya uwekezaji ukue.

Lakini sehemu kubwa ya wafanyabiashara wanahitaji fedha zaidi kuliko wanavyoweza kupata kukuza biashara zao kwa sababu mikopo ya benki ina gharama kubwa kutokana na kiwango kikubwa cha riba .

Njia pekee ya kupunguza pengo la kifedha kwa wengi walio katika biashara hizi, ni sekta binafsi, ikiwemo uwekezaji binafsi, kuwekeza katika fedha za mtaji, kukuza taasisi za kifedha na kupitia mpango wa uwekezaji wa pamoja na ushirikiano na makampuni makubwa.

Kukuwa kwa biashara pia kumefungua fursa za upatikanaji wa mitaji kupitia majukwaa ya ufadhili wa watu wengi na wa rika kwa rika, huku makampuni kama Auspicious Blockchain yamekuwa yakiunganisha wawekezaji waishio nje ya bara na wafanyabiahsara wengine.

Tatizo mara nyingi, ni kuwepo kwa pengo la kisheria, kati ya mwekezaji na mfanyabiashara wa kiafrika.

Kupitia kazi yetu Strand Sahara, tumebaini changamoto tatu za kisheria ambazo wafanyabiashara wa kiafrika wanakabiliana nazo:

Hawathaminiwi

Ni wafanyabiashara wachache mno ambao wanaweza kufaulu vigezo vinavyohitajika kufanya uwekezaji binafsi, hii mara nyingi inatokana na taarifa za kisheria na kifedha na kushindwa kufuata njia sahihi au muundo sahihi wa sheria za biashara.

Mapungufu haya, hupunguza thamani ya biashara, kwa sababu wawekezaji au wakopeshaji hawatakuwa na uhakika kwamba uwekezaji wao katika biashara utalindwa.

Hawana taarifa za kutosha

Wamiliki wa biashara mara nyingi wanakuwa hawana taarifa ya mahitaji ya ushirikiano, ikiwemo kuchagua mfumo sahihi wa kisheria kwa biashara, na kuingia katika makubaliano sahihi na washirika, wakurugenzi na hata waajiriwa.

Hii pia inaenda mbali zaidi, sheria nyengine za biashara zinazotoa ulinzi, kama kuwepo kwa mikataba ya biashara, makubaliano na waajiriwa, na ulinzi wa haki miliki.

Hii sio kikwazo pekee kwa wawekezaji, lakini pia ni sababu kubwa ya kuanguka kwa biashara.

Hawahudumiwi ipasavyo

Huduma za kisheria za kibiashara mara nyingi huonekanwa na wamiliki wa biashara kama upatikanaji wake ni wa taabu, haina thamani, huku msaada wa kisheria ukitafutwa dakika za mwisho.

Wanalalamika kwamba, inachukua muda mrefu sana kupata majibu wanayohitaji au kupata suluhu, huku wakiendelea kufanya kazi zao.

Mara nyingi pia wanakuwa hawana uhakika wa gharama itakayotumika kupata ufumbuzi wa matatizo yao, hii mara nyingi inakuwa ni zaidi ya matarajio yao.

Suluhu? Hakuna shaka kwamba wafanyabiashara wadogo na wa kati wanahitaji huduma za sheria ya biashara ili kuwaandaa kukuwa kifedha.

Kuna haja kubwa kwa wanasheria kutoa elimu kwa wamiliki wa biashara kuhusu umuhimu wa huduma hizi.

Wanasheria wanatakiwa wazingatie kutengeza bidhaa na huduma zitakazosaidia kubaini tatizo la kisheria katika biashara kabla tatizo halijatokea, kuonesha mapengo yaliyopo, halafu kuwaonesha jinsi ya kuziba mapengo hayo.

Mwishoni kabisa, wanasheria sharti watafute njia za kuhakikisha huduma hizi zinapatikana kwa wepesi, uwazi na kwa bei nafuu.

Suluhu moja wapo ni kwa wanasheria kutumia teknolojia kuunda mifumo ambayo inaweza kutumika kupitia njia ya mtandao kutoa suluhisho, kuwawezesha wafanyabiashara kuweza kupata huduma za kisheria kwa njia rahisi zaidi na ya uwazi bila kutumia gharama kubwa, ili waweze kukuza biashara zao, kufanikiwa kutengeza ajira na kukuza uchumi ambao unahitajika kwa kiasi kikubwa barani Afrika.

Hivyo ndivyo Strand Sahara ilivyodhamiria kufanya kupitia mtandao wetu http://www.strandsahara.com.