Joseph Irungu almaarufu Jowie alihukumiwa kifo na mahakama Kenya  mnamo Machi 13, 2024/ Picha: Wengine

Katika rufaa yake Jowie analalamika kuwa hukumu iliyotolewa na hakimu Grace Nzioka mnamo Machi 13, 2024, inakiuka haki zake za kikatiba.

Jowie ameielezea hukumu yake kama "mateso, ukatili, unyama" na udhalilishaji unaokwenda kinyume na ibara ya 25 ya Katiba ya Kenya.

Katika rufaa hiyo, Jowie anadai fidia kwa ukiukwaji wa haki zake chini ya Vifungu 27, 28, 29, 48 na 50 vya Katiba ya Kenya."

Kesi ya Joseph Irungu almaarufu Jowie ya mauaji nchini Kenya ilivutia hisia tofauti nchini humo. "Jowie" anashitakiwa kwa mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani.

Kesi ya mauaji ya Monica Kimani ilivura hisia nyingi nchini Kenya, haswa baada ya kuhusishwa na aliyekuwa mwanahabari maarufu nchini Kenya, Jacque Maribe.

Maribe, ambaye aliachiwa huru na mahakama, ndiye alyesoma habari za tukio hilo, kupitia televisheni ya Citizen TV ya nchi hiyo.

Jowie, 33, alipatikana na hatia ya mauaji ya Kimani, ambaye aliuawa kikatili katika nyumba yake ya Lamuria Gardens jijini Nairobi usiku wa Septemba 19, 2018.

Jaji Nzioka aliamua kwamba mauaji ya kutisha ya Monica Kimani yalikuwa "ya kukusudia."

Kesi hii ilivutia wengi kwani mpenzi wa Jowie wakati huo alikuwa mwandishi wa habari nchini humo mabaye ndiye alisoma habari hiyo ya mauaji ya mwanamke huyo.

Hukumu ya kifo ndiyo hukumu ya juu zaidi nchini Kenya na kwa kawaida, ina maanisha mhukumiwa anafaa kuuliwa kama adhabu inavyosema.

Rais ndiye peke mwenye uwezo chini ya sheria kuidhinisha kuuawa kwa mtu aliyehukumiwa kifo.

Hata hivyo tangu 1987 serikali haijaidhinisha mauaji ya mfungwa.

TRT Afrika