Rais wa Kenya William Ruto, akiwa na viongozi wa Afrika, akihutubia wanahabari baada ya kufungwa kwa Mkutano wa Kilele wa Hali ya Hewa barani Afrika (ACS) 2023 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta (KICC) jijini Nairobi, Kenya, Septemba 6, 2023. REUTERS/Moniah Mwangi

Viongozi wa nchi za Afrika wamehitimisha mkutano wao wa siku tatu wa Mabadiliko ya Tabia nchi huko jijini Nairobi nchini Kenya kwa kutoa azimio.

"Azimio la Nairobi" jinsi linavyoitwa limeitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka katika kupunguza hewa chafu.

Mkutano wa marais wa hali ya hewa barani Afrika umetaka mataifa yote kupunguza utoaji wa hewa chafu na kupunguza msongamano wa gesi chafuzi.Mkutano wa marais wa hali ya hewa barani Afrika umetaka mataifa yote kupunguza utoaji wa hewa chafu na kupunguza msongamano wa gesi chafuzi.

Katika Azimio hilo pia, Afrika imeomba mataifa yaliyoendelea kuheshimu ahadi ya kutoa dola bilioni 100 katika ufadhili wa kila mwaka wa hali ya hewa. Hii ilikuwa ahadi iliyotolewa miaka 14 iliyopita na mataifa yaliyoendelea katika mkutano wa Copenhagen.

"Tunawaomba viongozi wa dunia kuunga mkono pendekezo la serikali ya kimataifa ya uwepo wa ushuru wa kaboni ikiwa ni pamoja na ushuru wa kaboni kwenye biashara ya mafuta, usafiri wa baharini na anga," sehemu ya Azimio imesema.

Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh akipeana mkono na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir huku Rais wa Kenya William Ruto akicheka na Rais wa Ethiopia Sahle-Work Zewde kwenye mkutano na wanahabari baada ya kufungwa kwa Mkutano wa Hali ya Hewa barani Afrika (ACS) 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) ) jijini Nairobi, Kenya, Septemba 6, 2023. REUTERS/Moniah Mwangi

Mkutano huo umewataka kujitolea kwa mchakato wa haki na wa kasi wa kukomesha makaa ya mawe, na kukomesha ruzuku zote za mafuta.

Afrika inadai kuwe na mchakato mpya wa msamaha wa deni kwa wito wa mageuzi ya mfumo wa kimataifa wa kifedha na usanifu wa kifedha wa kimataifa.

Mkutano huo pia umeomba kuongezwa kwa muda wa deni ili kipindi cha msamaha cha miaka 10 kianzishwe kwa ulipaji wa deni.

Wakuu wa nchi za Afrika wamependekeza kwamba usanifu mpya wa ufadhili unaokidhi mahitaji ya Afrika uanzishwe.

Sauti za Wananchi

Watu wanatumia simu zao za mkononi kurekodi mkutano wa wanahabari baada ya kufungwa kwa Mkutano wa Hali ya Hewa barani Afrika (ACS) 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC), Nairobi, Kenya, Septemba 6, 2023. REUTERS/Monica Mwangi

Wakuu wa nchi walipokuwa wakisoma tamko lao jijini Nairobi, kundi la wananchi walikuwa wakikutana katika mojawapo ya makazi yasiyo rasmi katika kitongoji cha Mathare.

"Wanazungumza kwa niaba yetu lakini hawajui tunachohitaji," asema Humphrey Omukutu.

Omukutu anaongoza kikundi cha wakulima wa mijini kutoka katika makazi yasiyo rasmi ambao wanajiita "wakulima wa geto."

Pamoja na wakazi wengine kutoka katika makazi holela jijini walikutana ili kujipa moyo kwa kazi wanayoifanya.

"Sauti halisi ya Wakenya iko hapa, na katika maeneo mengine ya bara, iko katika makazi mengine yasiyo rasmi kama yetu," anasema Omukutu.

Omukutu anajivumia kuhamasisha kundi la vijana kupanda miti pembezoni mwa mto Nairobi, mojawapo ya mito ambayo kwa muda mrefu imechafuliwa.

Mjumbe kutoka jamii ya kiasili ya Wamasai akipiga pembe na kuvaa vazi la manyoya ya mbuni anapowasili kwa Mkutano wa Kilele wa Hali ya Hewa barani Afrika (ACS) 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Kenyatta (KICC) jijini Nairobi, Kenya, Septemba 6, 2023. REUTERS/Moniah Mwangi TPX PICHA ZA SIKU

"Watu kama sisi wa kawaida tunaelewa suluhisho la mabadiliko ya hali ya hewa kwa sababu tunaishi na athari za mabadiliko ya hali ya hewa kila siku," anasema.

"Kwenye mkutano wa kilele tunasikia wanatumia maneno makubwa kama vile "biashara ya kaboni," lakini ni jambo rahisi kwani ikiwa tunataka kusafisha hewa yetu tunapaswa tu kupanda miti Zaidi. Kwa nini viongozi wa Afrika hawawezi kufanya maamuzi ambayo yanawezesha jamii kama yetu kupanda miti zaidi?"

Omukutu na wanahaŕakati wengine wa mazingiŕa katika makazi yasiyokuwa ŕasmi wanasema ili azimio la Naiŕobi kuleta mabadiliko, ni lazima utekelezaji ujumuishe watu mashinani ambao wanahusika moja kwa moja katika miradi inayofanya mabadiliko.

TRT Afrika