Aubabe Moroo katika uhai wake | Picha: Barick Bwema

Alitumia maisha yake yote katika kijiji alipozaliwa cha Nderi eneo la Aru jimbo la Ituri Mashariki mwa Congo. Kulingana na maelezo yake, alizaliwa mwaka wa 1877 ambao mwezi na siku hazijulikani.

Moroo hakuorodheshwa na Guinness World Record kwa sababu aliishi katika eneo la mbali sana katika sehemu ya kaskazini ya DRC.

Guiness World Records ni kitabu cha orodha kinachotolewa kila mwaka, kikiorodhesha rekodi za ulimwengu za mafanikio ya wanadamu na hali ya kupita kiasi ya ulimwengu.

“Niliona picha zake kwenye mitandao ya kijamii tangu Disemba 2022 na sikujua kama tayari yuko Kinshasa – Wizara itatafuta taarifa zaidi na kurudi kwenu tatizo la nchi yetu kuna maeneo yapo mbali na ulimwengu na haiwezekani kwenda kuchunguza" alisema Mwanahabari Barick Bwema.

Kwa sasa, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Urithi nchini DRC haijathibitisha habari hiyo au umri wake kwa sababu hakuna ushahidi wa kisayansi wa kutosha kuthibitisha kuwa alizaliwa 1877.

Maeneo mengine yenye watu wazee zaidi Afrika Mashariki

Nchini Kenya, watu kadhaa wamedai kwenye mitandao ya jamii kuwa Julius Wanyondu Gatonga aliyezaliwa mwaka 1884, mwenye umri wa miaka 137 hivi leo, ndiye mtu mwenye umri mkubwa zaidi nchini humo lakini hayumo kwenye orodha ya rekodi ya dunia ya Guinness.

Mwanamke wa Kitanzania Bibi Nyikobe, kutoka Bunda mkoani Mara anadai kuwa na umri wa miaka 135 na kuwa mzee kuliko wote, lakini Ofisi ya Taifa ya Takwimu, NBS, nchini Tanzania haiwezi kuthibitisha.

NBS wameeleza TRT Afrika kwa njia ya simu kwamba hawawezi rekodi idadi hiyo ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 100 kutokana na uwezo wa mitambo kutohifadhi taarifa za watu waliozidi umri wa miaka 99.

Aubabe Moroo alikuwa amehamishiwa katika mji mkuu wa DRC Kishasa, tangu Januari mwaka jana 2022 baada ya picha zake na video kusambaa mtandaoni.

Lakini je unadhani kwa nini taarifa za watu wazee zaidi barani Afrika hazijaingizwa katika rekodi ya Dunia?

TRT Afrika