Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya Helikopta na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga wakati wakiangalia athari za mafuriko yaliyotokea katika mji mdogo wa Katesh pamoja na vijiji jirani, Hanang Mkoani Manyara. Picha/Ikulu
Raiswa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa amembeba mtoto Wina Joseph mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 8 ambaye pia yeye na mama yake ni waathirika wa mafuriko yaliyotokea Katesh Wilayani Hanang. Rais Samia aliwatembelea majeruhi wa maafa ya mafuriko hayo ambao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tumaini, Hanang Mkoani Manyara. Picha/Ikulu
Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na waathirika wa mafuriko waliopo kwenye kambi zao Katesh, Wilayani Hanang mkoani Manyara. Picha/Ikulu
Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye akiwa pamoja na viongozi wengine wakati wakimsikiliza rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Shule ya Msingi Katesh Mkoani Manyara. Picha/Ikulu