Nchi saba zaidi zaondolewa katika orodha ya ulipaji wa ada wakati wa kuingia nchini Kenya  / Photo: AFP

Mwezi Disemba 2023, Kenya iliondoa hitaji la visa kwa wageni wote wanaotembelea nchi hiyo.

Chini ya mfumo mpya, wasafiri wanaomba mtandaoni ili kupata idhini ya usafiri wa kielektroniki (ETA) na kulipa ada ya $30.

Serikali wakati huo iliondoa nchi za Afrika Mashariki kutoka katika Orodha hiyo zikiwemo Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rwanda, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda hazitahitajika kulipa ada ya $30, ili kupata idhini ya usafiri wa kielektroniki (ETA).

Na sasa serikali ya Kenya imeamua kuondoa nyengine saba katika ulipaji wa ada hiyo.

Comoros, Jamhuri ya Congo, Eritrea, Ethiopia , Mozambique, San Marino na Afrika Kusini.

"Raia wa nchi zifuatazo wameondolewa kwa ulipaji wa ada ya idhini ya kielektroniki baada ya kutuma maombi yao kupitia jukwaa la kidijitali la E citizen," serikali imesema katika mawasiliano kutoka kwa wizara ya mambo ya ndani.

TRT Afrika